Nyota
wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando amesema anatamani sana kuhamia
kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima
kutokana na mahubiri yake mazuri.
“Natamani
nihamie katika kanisa la Mchungaji Gwajima lakini mimi huwa napenda
kumuita Askofu kwa sababu ya upako alionao, naomba ikiwezekana na mimi
nihamie hapa,” alisema Rose.
Mwanamuziki nguli wa nyimbo za injili, Bongo Rose Muhando.
Katika
siku ambayo kulikuwa na sala ya shukurani kanisani kwa Gwajima Jumapili
iliyopita Kawe jijini Dar es Salaam, mchungaji huyo alimwambia Rose
aliyealikwa kuimba, kwamba yupo tayari kumjengea kanisa Dodoma anakoishi
na yeye mwenyewe alisimamie.
No comments:
Post a Comment