Jeshi
la polisi Jijini Mbeya linawashikilia wananchi wa kijiji cha Lupembe
Wilayani Kyela wapatao 93 kwa kuvamia shule ya sekondari Mwingo wakiwa
na silaha mbalimbali za jadi.
Wananchi
hao wamefanya uvamizi huo kwa kile kinachoelezwa kuwa walikuwa
wakiwataka walimu na wanafunzi wa shule hiyo waondoke katika eneo la
shule wanalodai kuwa ni mali ya kijiji.
Kwa
mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya Kamishana msaidizi wa
polisi Barakael Masaki amesema Chanzo cha fujo hizo ni Mgogoro wa mpaka
wa shule hiyo na eneo la kijiji.
dKamishana
Masaki ametoa wito kwa jamii kufuata sheria katika kudai haki zao kwa
njia ya amani na utulivu ili kuepukana na matatizo yanayoweza kuepukika.
No comments:
Post a Comment