
Atlètico Madrid wapo tayari kutoa pauni milioni 25
kuwasajili Javier Hernandez, 26 na Shinji Kagawa, 25, kutoka Manchester United
(Guardian), Barcelona wana wasiwasi wa kushindwa mbio za kumsajili Juan
Cuadrado, 26, ambaye anasakwa na Manchester United kwa pauni milioni 29 (Daily
Star), Liverpool na Tottenham wapo tayari kumfuatilia mshambuliaji kutoka Ivory
Coast Wilfried Bony, 25, wakati Swansea wakifikiria kuondoa kifungu cha
utenguzi cha pauni milioni 19 cha uhamisho (Daily Mirror), beki wa Arsenal
Thomas Vermaelen hatojadili mkataba mpya na Arsenal, katika jitihada zake za
kulazimisha uhamisho kwenda Barcelona au Manchester United (Sun), Everton bado
wanafikiria kuongeza wachezaji, na wanamfuatilia kiungo wa Manchester United
Tom Cleverly, 24 (Daily Mail), Tottenham wanakaribia kukamilisha kumsajili beki
wa kati kutoka Argentina, Mateo Musacchio, 23, kutoka Villareal na wapo tayari
kumuuza Younes Kaboul, 28, ambaye huenda akahamia Lazio kwa pauni milioni 6
(Telegraph), Pepe Reina huenda akabakia Liverpool baada ya AC Milan kushindwa
na mshahara anaotaka (Independent), Sunderland wapo tayari kumfuatilia Samuel
Eto'o ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Chelsea (Talksport), matumaini
ya Liverpool na Manchester United yamezizima baada ya kiungo Marco Reus
kusisitiza kuwa atabakia Borussia Dortmund msimu ujao (Metro), Louis van Gaal
ataamua wiki hii, nani anabaki na nani anaondoka wakati atakapokamilisha
mipango yake ya usajili na Ed Woodward. Javier Hernandez, Shinji Kagawa na
Marouane Fellaini huenda wakauzwa (Daily Telegraph), Liverpool wanapanda dau la
pauni milioni 5 kumtaka beki wa Barcelona Dani Alves, 31 (Mundodeportivo),
Arsenal wanajiandaa kutoa pauni milioni 23.9 kumsajili kiungo wa Sporting
Lisbon William Carvahlo (O Jogo), beki wa kulia wa Atlètico Madrid Javier
Manquillo amewasili Uingereza kufanya vipimo vya afya kabla ya kujiunga na
Liverpool (Daily Mail).
No comments:
Post a Comment