Thursday, 21 August 2014

Mario Balotelli transfer: Liverpool set to discuss personal terms after agreeing £16million fee

    The firebrand Italian looks set to join the Reds as a replacement for Luis Suarez and add further competition to Brendan Rodgers' attack

    Back to Britain: Balotelli is set to trade the red of Milan for Liverpool red
    Liverpool are this afternoon closing in on a deal for striker Mario Balotelli after agreeing to pay AC Milan £16million, reports James Pearce in the Liverpool Echo.
    The Reds have been granted permission by the Serie A outfit to discuss personal terms with the controversial Italy international, who is now expected to fly to Merseyside.
    Balotelli has confirmed to Sky Italia that he expects to imminently complete a transfer as he said: “This will be my last day at Milan.”
    Negotiations progressed quickly after Liverpool made their surprise move for the 24-year-old former Manchester City frontman.
    Their pursuit of Balotelli represents a remarkable U-turn after the club dismissed any interest in signing him earlier this month.
    Liverpool have been searching for a new striker since a deal to sign QPR's Loic Remy collapsed last month after the Frenchman failed a medical.
    The Reds enquired about the availability of Monaco’s Radamel Falcao, Paris Saint-Germain’s Edinson Cavani and Real Madrid’s Karim Benzema but were frustrated in their attempts to land a marquee signing.
    Brendan Rodgers had also considered signing Samuel Eto’o with the veteran striker a free agent after parting company with Chelsea at the end of last season.
    However, the Cameroon international was always viewed as a last resort and Liverpool have been actively pursuing other options.
    AC Milan v Manchester CityThat extensive search has led them to Balotelli, who is set to return to the Premier League 18 months after Man City sold him to Milan for around £16million.
    Then City boss Roberto Mancini showed Balotelli the door after growing tired of the striker’s antics.
    He was involved in numerous incidents during his three years at the Etihad Stadium, including setting fireworks off in his house and throwing a dart at a youth-team player.
    Balotelli also clashed frequently with team-mates and his manager on the training ground, running up a £340,000 fine.
    He scored 30 goals in 80 games in all competitions for City but only managed three in 20 matches during his final season there.

    Friday, 15 August 2014

    Viongozi wa Serikali na waganga wa jadi wahusishwa na mahuaji ya viungo vya Albino yanayoendelea nchini



     CHAMA cha watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania (TAS),kwa kushirikiana na Taasisi za kutetea haki za binadamu pamoja na jumuia ya watu wenye ulemavu,na shirika la UNDER THE SAME SAME (USS) wameitaka Serikali kusitisha vibali vya waganga wa  jadi ili kukomesha suala zima la ukataji waviungo vya albino.
     Mbali na agizo hili pia wameitaka serikali kusitisha matangazo ya waganga wa jadi kwa madai kwamba wanapotesha jamii huku matukio ya ukatili yakiendelea.
    Akizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Dar es Salaam Meneja Uendeshaji wa TAS Gamariel Mboya alisema wamesikitishwa na kitendo cha kinyama alichofanyiwa mtoto wa miaka 15 Upendo Sengerema cha kukatwa Mkono wa kulia wiki iliyopita   katika kijiji cha Usinge mkoa wa Tabora.
    Alisema tukio hilo ni la pili kutokea kwa kipindi cha miezi mitatu tangu kuanza kwa mwaka huu hali inayotishia amani ya kuishi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
    “Kuendelea kukithiri kwa vitendo hivi vya kikatili  ni ishara tosha kuwa kama hatua za makusudi hazitachukuliwa uovu huu wa ukatwaji wa viungo utaendelea  huku walengwa wakubwa wakiwa ni waganga wa kienyeji pamoja na viongozi wan chi,”alisema Mboya.
    Alisema imekuwa ni kawaida kila ifikapo kipindi cha uchaguzi matukio haya ya kikatili kuendelea kukua kwani ripoti ya uchunguzi inaonesha kuwa tangu mwaka 2006 mpaka sasa ni watu 73 waliouwawa ,watu 10 wamekatwa viungo, watu 46 walinusurika kukatwa na makaburi 18 yalifukuliwa.
    Alisema mpaka sasa watu wenye ulemavu wa ngozi wamekuwa wakiishi kwa hofu kubwa jambo ambalo liawaathiri kisaikolojia na linarudisha nyuma maendeleo.
    Alisema vitendo hivyo vya ukatwaji wa viungo unaonesha ni kwa kiasi gani serikali,wabunge pamoja na wanasiasa hwana nia ya dhati na utashi wa kisiasa ili kuweka mipango madhubuti na shirikishi ili kutathmini shughuli za waganga wa jadi.
       




    Waandishi wa habari wametakiwa kuacha kushirikiana na UKAWA



    WAANDISHI wa habari wametakiwa kuacha kushirikiana na Taasisi binafsi na wanasiasa wasiokuwa na nia njema ya kupatikana kwa katiba mpya.
    Tahadhari hiyo imetolewa na jana na Balozi wa Amani nchini, Risasi Mwaulanga aliyesema kuwa wapo baadhi ya wanasiasa wenye nia ya kuwapotezea Watanzania fursa ya kupata katiba mpya kwa maslahi yao binafsi.
    Akitolea mfano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema kwamba wamekuwa wakitumia vyombo vya habari vibaya kwa nia ya kupoteza fursa ya Watanzania kupata Katiba mpya.
    Alitoa wito kwa Ukawa kurejea bungeni kupambana kwa hoja na si kutumia propaganda za kupotosha umma.
    “Tangu walipoanza Ukawa wamejipambanua kwa kuonyesha kwamba wapo tofauti na malengo ya kupatikana kwa katiba huku kwa makusudi wamekuwa wakitumia vyombo vya habari kufaanikisha malengo yao,”alisema Mwaulanga.
    Alisema kuwa kipindi kilichopita katika bunge maalumu la Katiba Mbowe alishawahi kusema kwamba katiba mpya itapatikana kwa ngumi na mateke sasa cha kushangaza aanakuwa mstari wa mbele kupinga upatikanaji wa katiba hiyo.
    “Katika moja ya vikao vya bunge la katiba awamu iliyopita, Mbowe aliwahi kusema kuwa, ni lazima katiba ipatikane kwa ngumi au mateke. Lakini inashangaza leo kuwa mpingaji naamba mojaa wa kupatikana kwa katiba mpya huku akiwa anatetea maslahi binafsi.
    Mwisho.

    Wednesday, 13 August 2014

    Cristiano Ronaldo dedicates man of the match award to Sir Alex Ferguson following Real Madrid's Super Cup triumph


    For old times: Ronaldo dedicated his award to his former Manchester United bossCristiano Ronaldo dedicated his man of the match award to Sir Alex Ferguson after scoring twice in Real Madrid’s 2-0 victory in the European Super Cup against Sevilla.
    Ferguson was part of UEFA’s technical committee and named the former Manchester United forward man of the match after he won the Super Cup for the first time in his career.
    Ronaldo said: ‘I am happy because I scored these two goals and I want to thank Sir Alex for handing me the man of the match trophy.
    All smiles: Ronaldo briefly met with Ferguson shortly after he collected his Super Cup winners' medal
    ‘He helped me a lot when I was just 18 in Manchester and I want to say I respect him and thank him so much for everything he did in my career.
    ‘This was a trophy I wanted because I haven’t won it yet. I was nervous, but I managed to work well with the team and I am pleased.’
    Ferguson, who opted for the Cardiff City Stadium instead of Manchester United’s final pre-season friendly with Valencia at Old Trafford, admitted it was an easy decision to name him man of the match.
    Fergie said: ‘Normally in a cup final it is difficult to choose a man of the match but Cristiano made it easy for me.’
    Ronaldo, who was part of the Portugal team who made an early exit from the World Cup in Brazil, claimed new signings Toni Kroos and James Rodriguez have settled straight into life at the Bernabeu.
    He added: ‘These are two crucial players for us, they played well and helped the team win an important trophy. That’s why we are happy at Real Madrid to welcome them.
    ‘They are doing well and playing well. My team helped me and I am happy to score twice.’

    Cristiano Ronaldo amfunika Lionel Messi kwenye rekodi nyingine ya magoli ulaya


    Upinzani wa wachezaji bora wa kizazi hiki cha soka Cristiano Ronaldo na Lionel Messi umekuwa ukitawala vypmbo vya habari kila kukicha.
    Usiku wa jana kulikuwa na mchezo wa UEFA Super Cup kati ya mabingwa wa UEFA Europa League – Sevilla dhidi ya mabingwa wa UEFA Champions League – Real Madrid, mchezo amba ulipigwa jijini Cardiff, Wales.
    Matokeo ya mchezo huo ni ushindi wa 2-0 kwa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akifunga magoli yote mawili na kuandika rekodi nyingine kwenye soka barani ulaya.
    Magoli hayo ya Ronaldo yamemfanya atimize jumla ya magoli 70 kwenye michuano ya ulaya na hivyo kumpita Messi ambaye ana jumla ya magoli 68.
    Mpaka kufikia April 2012, nahodha wa Ureno alikuwa nyuma kwa magoli 18 kumfikia Messi, lakini ndani ya misimu miwili amefanikiwa kumfikia Messi na kumpita akifunga jumla ya mabao 29 ndani ya msimu miwili.
    Ronaldo sasa anakuwa amefunga magoli 68 kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya na mawili kwenye Super Cup, jumla 70, akiwa amemfikia nyota wa zamani Juventus na AC Milan Fillipo Inzaghi.
    Gwiji wa soka wa Real Madrid ndio mchezaji anayeongoza kwa magoli mengi barani ulaya akiwa ameziona nyavu mara 76.

    Urusi kuamishia msaada wa kijeshi Misri

    Rais Putin akimpokea Rais Al-Sisi, Sochi
    Rais Putin akimpokea Rais Al-Sisi, Sochi
    Rais wa Urusi, Vladmir Putin amekutana na mwenzake wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana kuhusu masuala ya ushirikiano mkubwa wa kijeshi, teknolojia na biashara huria.

    Rais Putin ameahidi kuharakisha hatua ya kupeleka silaha za mabilioni ya dola nchini Misri, na ameikaribisha nchi hiyo katika biashara huria. Viongozi hao wawili wameimarisha uhusiano wao tangu Putin alipomuunga mkono Al-Sisi wakati wa ziara yake mjini Moscow mwezi Februari, kipindi alichokuwa anagombea urais wa Misri.
    Putin amesema mwezi Machi mwaka huu nchi hizo mbili zilisaini itifaki zinazolingana na kwamba wanapeleka silaha nchini Misri na wako tayari kutanua ushirikiano huo.
    Aidha, Al-Sisi amemshukuru Rais Putin kwa kuwa kiongozi wa kwanza nje ya mataifa ya Kiarabu, kumualika tangu alipoapishwa kuliongoza taifa lake. Alisema watu wote wa Misri wanaifatilia ziara yake na wanategemea kuwepo kwa ushirikiano wa hali ya juu kati ya mataifa hayo mawili.
    Rais Al-Sisi akisalimiana na Rais Putin Rais Al-Sisi akisalimiana na Rais Putin
    Urusi imechukua jukumu la kupeleka silaha Misri, baada ya Marekani kusitisha kupeleka silaha kutokana na ukandamizaji uliofanywa na Al-Sisi baada ya kuiondoa madarakani serikali ya zamani ya Kiislamu, mwaka uliopita.
    Baada ya mkutano wa viongozi hao wawili, gazeti la kila siku la biashara la Urusi la Vedemosti limeripoti kuwa Urusi na Misri zimesaini mpango unaokaribia Euro bilioni 2.2 wa makombora na ndege za kivita, utakaofadhiliwa na Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu.
    Misri inapendelea zaidi mifumo ya ulinzi wa anga
    Mkuu wa kituo cha utafiti wa biashara ya silaha duniani mjini Moscow, Igor Korotchenko, amesema Misri inapendelea zaidi mifumo ya ulinzi wa anga. Amesema anadhani kusainiwa kwa mikataba halisi ni suala la muda tu na kwamba makubaliano katika ngazi ya kisiasa tayari yameshafikiwa.
    Ama kwa upande mwingine, Rais Putin ameikaribisha Misri kuanzisha ukanda wa biashara huru kati ya Misri na umoja wa ushuru na forodha wa Urusi, Belarus na Kazakhstan. Urusi imesema itaongeza kiwango cha kupeleka ngano nchini Misri na kuingiza bidhaa nyingine za kilimo kutoka Misri.
    Viongozi wa Urusi na Misri wakizuru kituo cha michezo ya kuteleza kwenye theluji, Sochi Viongozi wa Urusi na Misri wakizuru kituo cha michezo ya kuteleza kwenye theluji, Sochi
    Urusi inaangalia vyanzo vipya vya usambazaji wa bidhaa, baada ya wiki iliyopita kupiga marufuku chakula kutoka Marekani, Umoja wa Ulaya, Australia, Canada na Norway, ikiwa ni katika kujibu hatua ya vikwazo vilivyowekwa dhidi yake kutokana na mzozo wa Ukraine.
    Akizungumza baada ya kukutana na Rais Al-Sisi, Putin amesema tayari Misri imeongeza usambazaji wa bidhaa za kilimo kwenye soko la Urusi kwa asilimia 30 na iko tayari kuongeza asilimia nyingine 30 katika siku zijazo.
    Waziri wa Kilimo wa Urusi, Nikolai Fyodorov, amewaambia waandishi wa habari mjini Sochi kuwa kuongezeka kwa chakula kama vile viazi, vitunguu, vitunguu saumu na machungwa kutoka Misri, kutasaidia kufidia nusu ya upungufu wa bidhaa hizo uliosababishwa na hatua ya kupiga marufuku.

    Canada kutoa chanjo ya majaribio dhidi ya Ebola


    Serikali nchini Canada inasema kuwa itatoa hadi dosi 1,000 za chanjo ya majaribio ya ugonjwa wa Ebola kwa shirika la afya ulimwenguni WHO.
    Hii ni kwa elengo la kusadia kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Afrika ambao hadi sasa umewaua zaidi ya watu 1,000.
    Hatua hii ni baada ya shirika la afya duniani kusema ni sawa kimaadili kutumia dawa ambayo bado infanayiwa majaribio kutibu wagonjwa katika hali ya dharura.
    Waziri wa afya nchini canada Rona Ambrose amesema kuwa nchi hiyo imetengeneza karibu dosi 500 za dawa hio lakini haijafanyiwa majaribio kwa binadamu.
    Wataalamu wanaonya kuwa huenda ikachukua hadi miezi sita kuunda kiwango cha dawa ambacha kinaweza kutumiwa.
    Kamapuni moja wa kimarekani ambayo ilikuwa imetengeneza dawa za majaribio inasema kuwa kwa sasa kiwango cha dawa ilicho nacho ni kidogo.

    Tuesday, 12 August 2014

    Majambazi Yaua Baba na Mama na kumjeruhi mtoto wa Miezi 4

    Watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia na kuwaua mume na mke na kumjeruhi mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 4 aliyeachwa na mama yake aliyeuawa  katika tukio lililotokea kijiji cha Murvyagira wilayani Ngara mkoani Kagera Ijumaa ya Agost 08,2014.

     
    Kwa mujibu wa mtoto mkubwa wa marehemu amesema majambazi hao walivamia nyumbani kwao majira ya saa 3 usiku ambapo walitumia panga na jembe kuwaua baba na mama yake na kisha kuwapora Maharage gunia moja, Radio, Gunia la Karanga, Mabati na Fedha vitu ambavyo hadi sasa thamani yake haijajulikana, huku wahalifu hao wakitokomea kusikojulikana.
    Aidha baadhi ya wananchi walioongea na mwandishi wetu, wameomba juhudi ya kuimarishwa hali ya usalama na ulinzi wilayani Ngara izidishwe hasa wakati huu ambako matukio ya mauaji yamezidi kujitokeza.

    Cadema imewataka wazee washirikiane ili kutetea maslahi yao na Taifa

    MWENYEKITI  wa  Chama  cha  Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Temeke, Bernard Mwakyembe  amewataka wazee nchini kuongeza ushirikiano ili kutetea maslahi yao na taifa kwa ujumla kutokana na busara walizonazo.  
    Rai hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana,  wakati wa semina ya kutambua sifa za kiongozi bora iliyowakutanisha zaidi ya wazee 100.
    Mwakyembe alisema, hakuna jambo lolote linaloweza kufanikiwa bila ya kushirikisha kauli za wazee, hasa waliokuwa na busara katika utatuzi wa mambo mbalimbali ikiwemo migogoro katika vyama.
    “ Kauli ya wazee ni dawa, lakini kutokana na kuwa nyuma kwenye suala la kujitolea wanaonekana hawafai au wamepitwa na wakati, haya yote huenda yakatokana na wengi wao kutotambua sifa zao katika jamii inayowazunguka”alisema.
    Mwakyembe aliwahakikishia wazee hao kuwa, Chadema itasimamia haki zao juu ya kuzitambua sifa zao zitakazowasaidia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kuleta mabadiliko yatakayowainua kiuchumi.
    Hata hivyo, aliwafafanulia baadhi ya sifa anazostahiki kuwa nazo kiongozi kuwa, awaze mafanikio makubwa, awe na nia kwa jambo analotaka kuongoza, ajitambue mwenyewe, asimamie maamuzi sahihi asiwe kigeugeu pia adhibiti msongo wa mawazo.
    “Siku zote uongozi ni dhima kuna wale wanaozaliwa  na bahati hiyo huku wengine wakizisomea, lakini yote sawa hivyo kiongozi bora
    anatakiwa akubali kukosolewa, awe msikilizaji na afuate haki, pia anatakiwa atie moyo watu pamoja na kufurahia mafanikio”alisema.
    Alisema, kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wasaliti kutoka na kutozingatia sifa za uongozi ikiwemo kukubali lawama, kutoungana na watu wa chini yake, kushindwa kutatua matatizo, kutojifunza kutokana na makosa pamoja na kukosa uaminifu.
    Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wazee wilayani humo, Waziri Mkunguna aliwataka wazee wenzake kuhakikisha wanajitolea katika mambo mbalimbali ya kukiendeleza chama hasa kwa kuzingatia kanuni na sifa walizoambiwa.
    MWISHOO.

    Wassira kuwa mgeni rasmi katika maonesho ya tatu ya sayansi chipukizi



    Waziri wanchi ofisi ya Rais sera na uratibu, Steven Wassira anatarajiwa kufunga maonesho ya tatu ya wanasayansi chipukizi katika ukumbi wa mwalimu Julius Nyerere.
     Pia Vijana wametakiwa kuwekeza katika suala zima la utafiti wa kisayansi ili kuleta maendeleo katika nchi.
    Akizungumza na waandishi wa habari jana,Kaimu mwenyekiti wa Sayansi chipukizi,Stephen Nyangonde alisema vijana wanafursa kubwa ya kujiinua kimaendeleo endapo watajikita kwenye masuala ya kisayansi.
    “Kama vijana watajikita katika masuala ya sayansi watapata kujiinua kimaendeleo kwakuwa kuna fursa kubwa endapo watakuwa makini,”alisema Nyangonde.
    Hata hivyo Nyangonde aliwataka vijana  kutumia taaluma ya sanaa ili kuhamasisha utafiti wa kisayansi .

    Waziri muhongo awataka watanzania kuchangamkiai fursa zinazotolewa na China




    Wizara  ya Nishati na Madini  imetoa wito kwa watanzania kuchangamkia fursa za ufadhili wa masomo zinazotolewa na china ili kuweza kutumia elimu hiyo kwa maendeleo endelevu ya sekta za Nishati na Madini.
    Akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana,Waziri wa Nishati na Madini, professor Sospeter Muhongo alisema nafasi hizi zinapatikana kwa ushindani baada ya kutangazwa kwenye vyombo vya habari.
    Alisema vigezo vinavyo tumika katika  kupata ufadhili ni aina ya kozi aliyoisoma  mwombaji katiaka shahada ya kwanza au uzamili,chuo alicho soma shahada ya kwanza,kiwango  cha  ufaulu  katika shahada ya kwanza kuanzia GPA 3.0 na uwiano wa jinsia.
    “Nafasi hizi zinapatikana kwa ushindani baada ya kutangazwa kwenye vyombo vya habari ambapo vigezo vinavyotumika kupata kupata ufadhili ni aina ya kozi uliyoisoma mwombaji, ”alisema muhongo.
    Pia alisema kuwa Serikali ya china imetoa ufadhili  wa nafasi kumi (10) za masomo kwa watanzania katika ngazi ya shahada uzamili na uzamivu katika fani ya mafuta na gesi.
    Alisema katika shahada ya uzamili wamechaguliwa watanzania 9 kati ya 46 walioomba ufadhili ambapo  katika shahada ya uzamivu amechaguliwa mtanzania mmoja kati ya wanne walio wasilisha maombi.