
Winga huyo amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano na kuifanya klabu hiyo iwe imetumia kiasi cha pauni milioni 130 katika kipindi hiki cha usajili nakupelekea klabu hiyo ifufue matumaini ya kufanya vizuri chini kocha wake mpya Louis Van Gaal.
Di Maria ambaye amejiunga na Real Madrid 2010 akitokea benfica alikuwa mmoja kati ya wachezaji muhimu katika klabu hiyo msimu uliopita, ambayo ilifanikiwa kuwa bingwa wa ulaya kwa mara ya 10,lakini baadae winga huyo alikataa kusaini mkataba mpya na kuomba kuondoka katika klabu hiyo.
Maisha ya Di Maria yalikuwa mabaya zaidi na kufikia hatua ya kuondoka kipindi Real Madrid walipofikia hatua ya kumsajili Ton Kloos na James Rodriguez na kupelekea winga huyo kuanza visa katika mechi ya Super Cup baada ya kuingia uwanjani katika mechi hiyo akitokea benchi na kuonyesha utovu wa nidhamu na hatimaye uongozi pamoja na Rais wa klabu hiyo Florentino Perez kuamuru auzwe.
Licha ya ujio wake kuonekana kuwa mkombozi wa klabu hiyo baada ya kufanya vibaya na kupelekea kumfukuza kocha wake David Moyes msimu uliopita na matokeo mabaya yaliyopatikana msimu ulipoanza baada ya kufungwa na Swensea 2-1,kutoka sare na Sunderland huku wakifungwa 4-0 na MK DNs katika ligi ya Capital one.
Mbali na sifa za mchezaji huyo akifahamika kuwa anauwezo mkubwa wa kukokota mpira na kunyumbulika ipasavyo lakini mapungufu yake yanaweza yakawa kikwazo cha yeye kufanikiwa katika ligi kuu ya uingereza na kuwekwa katika orodha ya wachezaji wasiokuwa na baati kwenye ligi hiyo.Gazeti lako la bingwa linakuletea mapungufu matano ambayo Van Gaal anatakiwa kuya fahamu ikiwa pamoja na………………
Ni winga ambaye asilimia 90% ya maamuzi yake katika kutoa pasi au kupiga shuti akiwa uwanjani anapenda kutumia zaidi mguu wa kushoto kwa staili ya uchezaji yake inamfanya hasiwe mchezaji anayeweza kucheza namba zaidi ya moja kwa kuwa tayari ameonyesha uzaifu wa kuto kufanya vizuri akiwa eneo mojazaidi hata baada ya Sami Khedira alipokuwa majeruhi na kupelekea winga huyo kubadilishwa mara kadhaa lakini hakuonyesha kiwango cha kulidhisha ambapo kocha wa Real Madrid,Ancelotti ikamalazim kubadili mfumo ili aweze kumtumia mchezaji huyo.
Di Maria ambaye mashabiki wa mpira Argentina wanamtambua zaidi kwa jina la El Fideo hakuna ubishi kwa hili kwamba winga huyo anaujuzi mkubwa wa kumili mpira katika msitu wa wachezaji huku akitumia ufundi mkubwa kuwatoka mabeki wa timu pinzani lakini ni winga mwenye mapungufu linapokuja suala la kutoa pasi kwa wakati katika maamuzi sahii na kumlenga mchezaji sahii,mara nyingi winga huyo ucherewa kutoa pasi na pasi hiyo haifiki kwa wakati kwa mtu sahii.
Baada ya kuumia kwa Sami Khedira akiwa kiungo wa timu hiyo kocha Ancelotti akalazimika kumpanga Di Maria acheze kama kiungo huku akilazimika kubadilisha mfumo kutoka 4-2-3-1 mpaka 4-3-3 na kupelekea Di Maria kucheza kiungo huku aki jaribu kushambulia kwa kuwa alikuwa akicheza nyuma ya washambuliaji lakini haikuwa ni namba yake aliyozoea ambayo huwa anafanya vizuri na kujiamini endapo anacheza namba hiyo.
No comments:
Post a Comment