Hatua hiyo
ya kuahidi kujenga kituo hicho imekuja baada ya wafanyabiashara hao kutaka
kuandamana kwa madai ya kuhitaji maelezo kutoka kwa Meya wa Almashauri ya
Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, juu ya
kiasi cha milioni 250 zilitolewa na TAMISEMI kwa matumizi ya kujenga
kituo hicho cha daladala.
Akizungumza
na mwandishi wa MTANZANIA Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Abubakar Rakesh
alisema kuwa wamesitisha kuandamana kutokana na Mkuu wa mkoa kutoa ahadi ya
kuanza ujenzi ndani ya wiki moja na kuwataka
wawe watulivu.
“Tulishajiandaa kuandamana hadi ofisini kwa Meya kama tulivyoahidi wiki iliyopita lakini tulipata ujumbe kutoka
kwa Mkuu wa Mkoa na kutuita ofisini kwake na baada ya kumueleza tulichokusudia
akafanya mawasiliano na viongozi wa
Manispaa ya Ilala na kutuahidi ndani ya wiki moja ujenzi utaanza,”alisema Rakesh.
Alisema
baada ya kamati ya mipango miji itakaa kikao leo na cha kuamua kazi hiyo ya
ujenzi itaanza lini ikiwa mkandalasi
alikuwa anataka kiasi cha
shilingi Milioni 350 huku zilizokuwepo ni
Milioni 250 lakini aliaidi kuongeza na kufikia fedha zilizokuwa
zinaitajika.
Ikumbukwe kuwa madai ya wafanyabiashara hao
yanakalibia miaka minne sasa tangu walipoanza kulala mika kuhusu miundo minu ya
jengo hilo pamoja,lakini kukwazo kikubwa kilidaiwa ni Meya wa Almashauli wa
Manispaa wa Ilaa na baadae wakakutana na Waziri mkuu ndipo mwanzoni wa mwaka
huu kiasi cha shilingi Milioni 250 zilitumwa na TAMISEMI kwenda Manispaa ya
Ilala ambapo mpaka sasa matumizi ya
fedha hizo hayaonekani.
No comments:
Post a Comment