Wednesday, 3 September 2014

Mambo husiyo yajua kuhusu Mario Mandzukic




Muda simrefu  mashabiki  wa mpira watafahamu kwanini  Diego Semeone alimuuza Diego Costa na kumsajili Mario Mandzukic (27), na Antonio Griezmann ili kuimarisha  safu ya  mshambuliaji  wa timu yake ya   Atletico Madrid.
Mandzukic amefanikiwa kuanza vyema baada ya kuifungia klabu yake bao la ushindi na kuweza kunyakuwa kombe la Super Cup baada ya Atletico kuifunga bao 1-0 timu  ya Real Madrid.
 Akithibitisha  ubora wake  na mafanikio makubwa aliyoyapata katika timu ya Bayern Munich ambapo amefanikiwa kuwa bingwa wa Ulaya 2013/14 akiwa katika timu hiyo kwa kutoa mchango mkubwa baada ya kufunga bao ambalo liliisaidia timu yake na kufanikisha ubingwa huo.
Bao hilo liliweza kumsahwishi kocha wa timu hiyo Pep Guardiola kujenga imani na mshambuliaji huyo kwa kuifunga  timu ya Borussia Drtmund. 
MAISHA YAKE
Mandzukic amezaliwa Mei 21/1986 katika mji mdogo uliopo ndani ya nchi ya Croatian uitwao Slavonski Blod  ukiwa umepakana na mpaka wa Bosnia  huku mji huo ukiandamwa na vita vya mara kwa mara vya mwaka 1992 na hatimaye  familia ya mshambuliaji kuamua kuhama ikiongozwa na baba yake mzee Mato alinukuliwa akisema “kitu cha msingi kwa familia yangu  ni usalama,eneo hili tunashuhudia kila siku watu wakifa kwa vita inayoendelea  kutokana na hali hiyo hatuwezi kuendelea kuwepo hapa  hatuwezi hata kidogo tunatakiwa kuondoka ili kuyanusuru maisha yetu,”.
HARAKATI ZAKE  KATIKA SOKA.
Baada ya kuondoka Crotia katika harakati za kutafuta usalama ndipo safari ya familia yake  ikafika  eneo la Ditzingen Ujerumani karibu na mji wa Stuttgart  hapo ndipo kipaji cha mshambuliaji huyo kikaanza kuonekana na alipofika miaka sita baba yake anayejulikana kwa jina la  Mato akaamua kumpeleka katika kituo cha  mpira cha watoto cha TSF Ditzingen na kufanikiwa kujiunga.
  
SAFARI YAKE YA KURUDI CROTIA
Mwaka 1996 familia yao ilikataliwa kupata ruhusa ya  kuendelea kuishi katika ardhi ya Ujerumani na kutimkia katika visiwa vya Baklans pembezoni mwa nchi hiyo ambapo ilipokonywa umiliki wa eneo hilo baada ya vita vya pili vya dunia.
Hata  hivyo  mshambuliaji huyo na mipango yake kucheza mpira akiwa katik timu ya NK Marsonia kabla ya kurudi Crotia na kujiunga na timu ya NK Zagred  baadae msimu wa usajili wa 2007 akafanikiwa kujiunga na timu kubwa Dinamo Zagreb kwa pauni milioni 1.3 baada ya kuuzwa mshambuliaji wa timu hiyo Eduardo da silva  .
KIPINDI KIZURI KATIKA MAISHA YAKE
Baada ya  Edin Dzeko kujiunga na Man City Januari 2011,ndipo nyota ya Mandzukic ikaanza kungaa katika timu hiyo ya Wolfsburg akithibitisha kipaji chake msimu wa 2011/12 akifunga mabao 12 na kutoa pasi 10 zilizo kuwa na matokeo ya mabao, akimaliza  huku akitajwa kuwa mmoja wa wafungaji bora wa mashindano ya Euro 2012  na kupelekea   timu  kubwa kama Bayern Munich kumuhitaji ambapo  Rais wa timu hiyo Uli HeneB alisikika akisema “timu yetu inatakiwa tuwe na mshambuliaji kama Mandzukic kwa napenda anavyo cheza” na kupelekea kusajiliwa baada ya timu yake ya taifa kutolewa na Ukraine katika mashindano  ya Mataifa   yaliokuwa yakifanyika nchini Poland.
SUPER MARIO WANAKUTANA
Katika msimu 2011/12  Mandzukic  alifanikiwa kuifungia timu yake ya taifa na klabu jumla ya mabao 45 na  kukaribisha ushindani mkali kutoka kwa Mario Gomez ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ndio mshambuliaji  namba moja wa  timu hiyo.
Kitendo cha kuumia kwa Gomez kikafungua ukulasa mpya kwa Mandzukic na kupelekea kuwa mshambuliaji wa kutegemewa katika timu hiyo huku akionyesha uwezo mkubwa katika Supercup dhidi ya Dortmund  na kumfanya Gomez asubili katika benchi akingoja aingie kama mchezaji wa akiba akimaliza ligi akiwa  na mabao 15.

ANAYEVUTIWA NAE ZAIDI
Akiwa katika timu ya NK Marsonia pamoja na  Ivica Olic ambaye wanacheza timu moja ya Crotia pia akicheza katika timu ya Hertha Berlin na Hamburger  SV kabla ya kujiunga na Bayern 2009 na Mandzukic akumtaja Olic kuwa ndiye anamvutia zaidi katika suala zima la uchezaji mpiara hali ilipelekea Mandzukic kukili kuwa akisema “Najua alikuwa akipendwa na mashabiki hapa ,”na kuongeza kuwa Olic alikuwa akifanya juudi kubwa kuakikisha anakuwa bora wakati wote  hivyo angependa kufanya alichofanya akiwa na timu hiyo.

MAPENZI YAKE KWA TIMU ZA UJERUMANI
Miaka minne aliyotumia akiwa  katika timu ya Baden- Wurttemberg ilimfanya kupenda kuendelea kuishi katika nchi ya Ujerumani  na kupelekea kukataa kujiunga na baadhi ya timu kutoka England na Ufaransa  kipindi cha usajili 2010 na kujiunga na Wolfsburg na baadae   Bayern 2012 akisema “Ujerumani ni nyumbani pia najiisi fuaraha nikiwa hapa ”.

MALENGO YAKE
Ili mshambuliaji aweze kuwa katika kiwango bora na kuzivutia baadhi ya timu kubwa ni mara nyingi anapimwa katika uwezo wake wa kufunga  mabao lakini Mandzukic ameonyesha ubora wake katika hilo na kutengeza nafasi nyingi za mabao na kufanikiwa na kila kitu kinachotakiwa katika kucheza mpira akiwa kama mshambuliaji.

“Najiona mpya kila nikiwa uwanjani endapo  nikiwa nje ya uwanja najiisi bado naitaji kupambana ili kushinda na kuleta changamoto,”alisema Manduzukuic.

MAISHA BINAFSI

Nimshambuliaji ambaye hapendi kuwa karibu na vyombo vya ukilinganisha na wengine kwani maisha yake yamekuwa tofauti akiwa na mpenzi wake Ivana na mbwa wake kipenzi Lene huku akitembelewa mara kwa mara na dada yake Ivana aliyeamia
ujerumani 2007 mwenye jina linalo fanana na mpenzi wake.

No comments:

Post a Comment