Man United wamethibitisha
kupokea kiasi cha pauni milioni 1.5 kwa mkopo wa muda mrefu wa Chicharito kutoka
kwa Real Mdrid badala ya pauni milioni 17.4 ambayo walioiitaji wamuuze jumla.
Chicharito ambaye
alijiunga United 2010 lakini mara nyingi alikuwa akitumika kama mchezaji wa
akiba akitokea benchi hali hiyo ilitishia kipaji chake ambapo katika kipindi
cha David Moyes alifanikiwa kuanza katika kikosi cha kwanza mara sita.
Kwamujibu wa taarifa ya
mtandao wa timu hiyo ilisema kuwa Javier Hernendez amejiunga Real Madrid kwa
mkopo wa muda mrefu huku ikiwa mara kwanza kwa timu ya Madrid kusajili
mshambuliaji kwa mkopo.
Mshambuliaji mwingine
ambaye anategemewa kuondoka katika timu hiyo ni Danny Welbeck ambapo
anatarijiwa kujiunga na Tottenham muda wowote kabla ya msimu wa usajili
kumalizika leo saa sita usiku.
Hata hivyo kunaripotiwa kuwa
kuondoka kwa Chicharito kumefungu milango ya mshambuliaji Falcao ambaye amejiunga
na Man United kwa mkopo wa mwaka mmoja
No comments:
Post a Comment