JUMLA ya shilingi billion 7.4 zimetengwa
kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya
Dawa (MSD) ujenzi unaotarajiwa kukamilika mwanzoni mwaka 2015.
Mbali na fedha hizo mpaka sasa
tayari ujenzi huo umekamilika kwaasilimia 51 huku kiasi cha shilingi bilioni 3.7
kimeshalipwa ikiwa ni shemu ya utoaji wa fedha za ujenzi wa jengo hilo.
Akizungumza na Mtanzania Meneja
Utawala wa (MSD) Johnson Mwakalitoko alisema
jengo hilo lenye ghorofa nne linalojengwa
na kampuni ya China Railway Jianchang Engeneering CO. T Limited litakuwa na
ofisi za watumishi, vyumba vya mikutano mikubwa na ya kawaida, maktaba, chumba
cha kuhifadhia nyaraka muhimu za kumbukumbu, eneo maalumu la kuegeshea magari
pamoja na eneo jingine kwaajili ya kuhifadhi mapipa ya maji.
Alisema kutokana na shuguli za
ujenzi kwenda kwa haraka ni matarajio yao kwamba januari 2015 ofisi hiyo
ityakuwa imeshakamilika.
Kwa upande Mwenyekiti Bodi Prof.
Idris Mtulia ameipongeza menejimenti ya MSD kwa kazi hiyo ya ujenzi na kuiagiza
menejimenti kuhakikisha ujenzi unasimamiwa kikamilifu ili uweze kukamilika
katika muda uliopangwa kwenye mkataba.
“Imekuwa ni kawaida kwa kampuni za
ujenzi kuahidi ujenzi utakamilika katika kipindi fulani mwisho wa siku haukamiliki
hiyo si halali kabisa,ni vyema kuwa makini na kukamilisha ujenzi kwa wakati,”alisema
Mtulia.
Mwishoo.
No comments:
Post a Comment