Muda simrefu mashabiki
wa mpira watafahamu kwanini Diego
Semeone alimuuza Diego Costa na kumsajili Mario Mandzukic (27), na Antonio
Griezmann ili kuimarisha safu ya mshambuliaji wa timu yake ya Atletico Madrid.
Mandzukic amefanikiwa kuanza vyema baada
ya kuifungia klabu yake bao la ushindi na kuweza kunyakuwa kombe la Super Cup
baada ya Atletico kuifunga bao 1-0 timu ya Real Madrid.
Akithibitisha ubora wake na mafanikio makubwa aliyoyapata katika timu
ya Bayern Munich ambapo amefanikiwa kuwa bingwa wa Ulaya 2013/14 akiwa katika timu
hiyo kwa kutoa mchango mkubwa baada ya kufunga bao ambalo liliisaidia timu yake
na kufanikisha ubingwa huo.
Bao hilo liliweza kumsahwishi kocha
wa timu hiyo Pep Guardiola kujenga imani na mshambuliaji huyo kwa kuifunga timu ya Borussia Drtmund.
MAISHA
YAKE
Mandzukic amezaliwa Mei 21/1986
katika mji mdogo uliopo ndani ya nchi ya Croatian uitwao Slavonski Blod ukiwa umepakana na mpaka wa Bosnia huku mji huo ukiandamwa na vita vya mara kwa
mara vya mwaka 1992 na hatimaye familia
ya mshambuliaji kuamua kuhama ikiongozwa na baba yake mzee Mato alinukuliwa
akisema “kitu cha msingi kwa familia yangu
ni usalama,eneo hili tunashuhudia kila siku watu wakifa kwa vita
inayoendelea kutokana na hali hiyo
hatuwezi kuendelea kuwepo hapa hatuwezi
hata kidogo tunatakiwa kuondoka ili kuyanusuru maisha yetu,”.
HARAKATI
ZAKE KATIKA SOKA.
Baada ya kuondoka Crotia katika
harakati za kutafuta usalama ndipo safari ya familia yake ikafika eneo la Ditzingen Ujerumani karibu na mji wa Stuttgart hapo ndipo kipaji cha mshambuliaji huyo
kikaanza kuonekana na alipofika miaka sita baba yake anayejulikana kwa jina la Mato akaamua kumpeleka katika kituo cha mpira cha watoto cha TSF Ditzingen na
kufanikiwa kujiunga.
SAFARI YAKE YA KURUDI CROTIA
Mwaka 1996 familia yao ilikataliwa
kupata ruhusa ya kuendelea kuishi katika
ardhi ya Ujerumani na kutimkia katika visiwa vya Baklans pembezoni mwa nchi
hiyo ambapo ilipokonywa umiliki wa eneo hilo baada ya vita vya pili vya dunia.
Hata
hivyo mshambuliaji huyo na
mipango yake kucheza mpira akiwa katik timu ya NK Marsonia kabla ya kurudi
Crotia na kujiunga na timu ya NK Zagred
baadae msimu wa usajili wa 2007 akafanikiwa kujiunga na timu kubwa
Dinamo Zagreb kwa pauni milioni 1.3 baada ya kuuzwa mshambuliaji wa timu hiyo
Eduardo da silva .
KIPINDI
KIZURI KATIKA MAISHA YAKE
Baada ya Edin Dzeko kujiunga na Man City Januari
2011,ndipo nyota ya Mandzukic ikaanza kungaa katika timu hiyo ya Wolfsburg
akithibitisha kipaji chake msimu wa 2011/12 akifunga mabao 12 na kutoa pasi 10
zilizo kuwa na matokeo ya mabao, akimaliza huku akitajwa kuwa mmoja wa wafungaji bora wa
mashindano ya Euro 2012 na kupelekea timu
kubwa kama Bayern Munich kumuhitaji ambapo Rais wa timu hiyo Uli HeneB alisikika akisema
“timu yetu inatakiwa tuwe na mshambuliaji kama Mandzukic kwa napenda anavyo
cheza” na kupelekea kusajiliwa baada ya timu yake ya taifa kutolewa na Ukraine
katika mashindano ya Mataifa yaliokuwa yakifanyika nchini Poland.
SUPER
MARIO WANAKUTANA
Katika msimu 2011/12 Mandzukic
alifanikiwa kuifungia timu yake ya taifa na klabu jumla ya mabao 45
na kukaribisha ushindani mkali kutoka
kwa Mario Gomez ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ndio mshambuliaji namba moja wa
timu hiyo.
Kitendo cha kuumia kwa Gomez
kikafungua ukulasa mpya kwa Mandzukic na kupelekea kuwa mshambuliaji wa
kutegemewa katika timu hiyo huku akionyesha uwezo mkubwa katika Supercup dhidi
ya Dortmund na kumfanya Gomez asubili
katika benchi akingoja aingie kama mchezaji wa akiba akimaliza ligi akiwa na mabao 15.
ANAYEVUTIWA NAE ZAIDI
Akiwa katika timu ya NK Marsonia
pamoja na Ivica Olic ambaye wanacheza
timu moja ya Crotia pia akicheza katika timu ya Hertha Berlin na Hamburger SV kabla ya kujiunga na Bayern 2009 na Mandzukic
akumtaja Olic kuwa ndiye anamvutia zaidi katika suala zima la uchezaji mpiara
hali ilipelekea Mandzukic kukili kuwa akisema “Najua alikuwa akipendwa na
mashabiki hapa ,”na kuongeza kuwa Olic alikuwa akifanya juudi kubwa kuakikisha
anakuwa bora wakati wote hivyo angependa
kufanya alichofanya akiwa na timu hiyo.
MAPENZI
YAKE KWA TIMU ZA UJERUMANI
Miaka minne aliyotumia akiwa katika timu ya Baden- Wurttemberg ilimfanya
kupenda kuendelea kuishi katika nchi ya Ujerumani na kupelekea kukataa kujiunga na baadhi ya
timu kutoka England na Ufaransa kipindi
cha usajili 2010 na kujiunga na Wolfsburg na baadae Bayern
2012 akisema “Ujerumani ni nyumbani pia najiisi fuaraha nikiwa hapa ”.
MALENGO
YAKE
Ili
mshambuliaji aweze kuwa katika kiwango bora na kuzivutia baadhi ya timu kubwa
ni mara nyingi anapimwa katika uwezo wake wa kufunga mabao lakini Mandzukic ameonyesha ubora wake
katika hilo na kutengeza nafasi nyingi za mabao na kufanikiwa na kila kitu
kinachotakiwa katika kucheza mpira akiwa kama mshambuliaji.
“Najiona mpya kila nikiwa uwanjani
endapo nikiwa nje ya uwanja najiisi bado
naitaji kupambana ili kushinda na kuleta changamoto,”alisema Manduzukuic.
MAISHA
BINAFSI
Nimshambuliaji ambaye hapendi kuwa
karibu na vyombo vya ukilinganisha na wengine kwani maisha yake yamekuwa
tofauti akiwa na mpenzi wake Ivana na mbwa wake kipenzi Lene huku akitembelewa
mara kwa mara na dada yake Ivana aliyeamia
ujerumani 2007 mwenye jina linalo
fanana na mpenzi wake.