Monday, 11 August 2014

Maliki kupambana mahakamani, kuulinda wadhifa wake dhidi ya Rais mpya wa Iraq


 
Waziri Mkuu wa Iraq Nouri Al Maliki anapeleka vita vyake vya kuuulinda wadhifa wake mahakamani, baada ya kutangaza kwamba atachukua hatua za kisheria dhidi ya rais mpya wa nchi hiyo, Fuad Massoum, kwa kukiuka katiba, kutokana na kushindwa kumpa waziri mkuu kutoka kundi kubwa zaidi la wabunge bungeni jukumu la kuunda serikali, mpya.
"Rais fuad Massoum hana haki kuchelewesha uteuzi wa waziri mkuu kutokana na matokeo ya uchaguzi uliopita, hali hii itazidisha matatizo ya kiusalama, ndio maana serikali inakwenda kotini kumshaki rais kwa kukiuka katiba," alisema Maliki.
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry na Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al Maliki.
Hata hivyo mahakama ya juu nchini humo imemuunga mkono Maliki katika harakati zake za kutaka kuiongoza tena nchi hiyo kwa muhula wa tatu.
Vyombo vya habari nchini humo Mahakama hiyo imeamua kwamba kulingana na sheria muungano wa Maliki walio wengi bungeni ndio walio na haki ya kupema jukumu la kuunda serikali, kwa hiyo rais Fouad Massoum atakuwa hana budi ila kumpa Maliki jukumu la kuunda serikali mpya.
Kwa upande wake Marekani inayounga mkono hatua ya rais mpya imesema inatumai Nouri al Maliki hataingilia siasa za nchi hiyo.
Marekani kupitia waziri wake wa mambo ya nje John Kerry imesema kuundwa kwa serikali ni hatua muhimu ya kuwepo kwa udhabiti na usalama nchini humo huku akiongeza kwamba kitu wananchi wanachokitaka kwa sasa ni amani kwa hiyo nguvu kupita kiasi hazipaswi kutumiwa na makundi ya kisiasa wakati huu wa kipindi cha demokrasia kwa Iraq

Njemba labaka mtoto wa mwaka mmoja jijini Arusha

MWAKAMtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja anayetambulika kwa jina moja la Devota wa Sokoni One jijini Arusha, amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kufuatia kubakwa na njemba moja iitwayo Rajabu Mkoba (30), mkazi wa eneo hilo.
 
Tukio hilo lilitokea Jumapili ya Agosti 3, mwaka huu ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kumbaka mtoto huyo kwa saa 9 na alimrejesha nyumbani kwa mama yake usiku wa manane.

Akizungumza na mwandishi, mama wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la  Mwitango alisema siku ya tukio, asubuhi alimkabidhi mtoto wake kwa jirani yake aliyemtaja kwa jina la Mustafa Kabananga na yeye kwenda kwenye kikundi cha akina mama.
 
Usiku saa mbili alikwenda kwa jirani yake huyo kumchukua mtoto wake lakini akaambiwa alichukuliwa na Rajabu.
 
“Nilikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa, yeye anaishi na wazazi wake. Hata hivyo, sikumkuta mwanangu wala mtuhumiwa, nikarejea nyumbani.

“Lakini kabla sijarudi, nilimwambia mama wa mtuhumiwa kuwa mwanaye kaondoka na mtoto wangu akaniambia  nirudi nyumbani nikaendelee kumtafuta nikimkosa niende kwake ili akajue cha kufanya, aliamua kwenda polisi’’ alisema mwanamke huyo.
 
“Ilikuwa saa 9 usiku nikiwa narejea nyumbani kutoka polisi, nilimkuta mama mzazi wa mtuhumiwa akiwa na mtoto wangu akimrejesha kwangu lakini mtuhumiwa hakuwepo.

“Niliamua kumchunguza vizuri mwanangu ndipo nilipogundua kuwa sehemu zake za siri zimevimba kupita kiasi huku damu zikimtoka.
 
“Nilikwenda kumweleza mama yake jinsi mwanaye alivyomtenda mtoto wangu na kumwachia mtoto ampeleke hospitali, alinisihi nisitoe taarifa za tukio hilo popote na akaniahidi kunipa shilingi laki moja,” alisema mama huyo.
 
Imeelezwa kuwa mama wa mtuhumiwa baada ya kukabidhiwa mtoto huyo hakumpeleka hospitali badala yake alikuwa akimtibu kwa kutumia miti shamba.

Baadhi ya majirani walikerwa na kitendo cha mwanamke huyo ambapo walimvamia na kumtolea maneno makali ya kumtaka alifikishe suala hilo kwenye vyombo vya sheria.
 
Kufuatia kelele za majirani ndipo alipokubali kurudi Kituo cha Polisi cha Unga Ltd ambapo polisi walifika nyumbani kwa mama wa mtuhumiwa na kumchukua mtoto huyo kisha kumwandikia hati ya matibabu (PF3) na kumpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya Mount Meru ambako anatibiwa.
 
Polisi hao walifungua jalada la mashtaka la kubaka na kunajisi lenye namba Ung/RB/2473/2014, bado mtuhumiwa hajakamatwa kwani alikimbia baada ya tukio hilo lakini mama yake ameshikiliwa kwa mahojiano .

Mtu mmoja auawa kikatili kisha mwili wake kuchomwa moto na watu wasiofahamika Morogoro

mwiliMtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja ameuwawa kikatili kisha mwili wake kuchomwa moto na watu wasiofahamika  katika eneo la mkundi manispa  ya Morogoro.
Kwa mujibu wa wananchi walishuhudia tukio hilo  wamesema wameshuhudia kundi la madereva wa pikipiki wakimshusha mtu huyo kisha kummwagia mafuta ya taa na kumchoma moto ambapo wameomba jeshi la polisi kufuatilia tukio hilo walohusika wachukuliwe hatua.
Wananchi wakazi wa  kata ya mkundi  wamesema hilo sio tukio la kwanza kutokea kwa watu kuuwawa na kisha kuchomwa moto na kuomba vyomba vya sheria kufanya kazi zake kwani huenda matukio hayo yanatokana na watu kuchoshwa na baadhi ya matukio ya wizi ambayo watuhumiwa huachiwa huru na vyombo vya sheria pasipo kuchukuliwa hatua.
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa  tukio hilo .

Sunday, 10 August 2014

The 7 Worst Mistakes People Make In Their 30s




Your 30s are typically a time for settling down after using your 20s to take risks and find yourself.
Many 30-somethings are busy raising a family and rising through the hierarchy at work.
Those who have already been through that decade say that as their responsibilities accumulated, it became easier to neglect relationships and ignore opportunities that they would never get again.
Quora users discussed lessons they learned in the thread: "What is the biggest mistake you made in your 30s and what did you learn from it?"
We've collected some of the best responses:
They abandon their loftier aspirations.
Twenty-somethings are often willing to settle for a job they are not passionate about, but before they know it, that job turns into their career. An anonymous poster writes that his or her biggest mistake of his or her 30s was to become "addicted to a monthly salary," in the sense that he or she settled for job security over career satisfaction.
If you've ever wanted to start a business or pursue a side project, it will only get more difficult as your responsibilities increase.
They put their career ahead of family and friends.
"Don't just work. Make memories. The older you get, the harder it is to make meaningful relationships. Foster those while you're young," writes Microsoft product designer Michael Dorian Bach, who is now in his late 30s.
They neglect their health.
Bach writes that the pursuit of a career can also be a drain on one's health. "Be healthy. That is priority 1. Don't get into your 30s being slow and tired all the time. It sucks," he says. Develop an exercise routine, and enjoy your mobility while you're still young.
They miss the chance to have kids.
CEO coach Alison Whitmire shares a personal story about how she took getting pregnant for granted in her 30s and chose to pursue a new career opportunity instead of trying to have a child. Years later, after a failed pregnancy and then a failed marriage, she remarried and had a baby at 43. She realizes now that no one is ever adequately prepared to have a child, and if you want one, it's best to do so before it's too late.
They don't spend enough time with their aging parents.
Entrepreneur and blogger James Altucher, who is now 46, writes about a particularly difficult memory for him: "When I was 34 I hung up the phone on my dad in an argument and never returned his calls. Six months later he had a stroke and died. A week before that he had emailed me to say hello but I didn't return the email. I'm sorry, Dad."
It can be easy to forget that your parents grow older as you do. Don't take them for granted.
They don't set up a financial foundation for the future.
Altucher writes about the many times in his 30s he bet practically all of his money on a business venture and then lost all of it. Altucher is doing well now, but he looks back on his failures as the result of recklessness. 
As your responsibilities grow, it can seem like what you put into savings won't amount to much come retirement, but it will only become harder to start saving in your 40s.
They stop having fun.
Just because you're not in your 20s anymore doesn't mean you need to give up enjoying life. Bach says he spent the early half of his adult life chasing money, and it only made him unhappy and more cynical about life.
Go on dates with your significant other. Take your kids on trips. Go to concerts with your best friends. Just don't forget that the money you work to make is useless if you're miserable.

Arsenal 3-0 Man City: 5 things we learned from the Community Shieldd




As Arsenal hammered Man City in the season's traditional curtain-raiser, we take a look at what we can conclude from our afternoon at Wembley

Arsenal won their first piece of silverware this season, beating Manchester City 3-0 to claim the Community Shield at Wembley.
Santi Cazorla netted the opener before Aaron Ramsey doubled their lead before half-time.
Substitute Olivier Giroud scored a stunner from distance to put the game beyond a weakened Manchester City side, who were missing the likes of Vincent Kompany, Bacary Sagna, Sergio Aguero and Pablo Zabaleta.
And here are five things we learned from the Community Shield. .
We can't take too much from this
The lost Boy: The likes of Boyata won't be featuring when it really matters  
Arsenal were by far the better side and deserved to win by a margin, but it would be foolish to read too much into a game where both sides were missing plenty of first-choice players.
Nobody expects Dedryck Boyata to start when Manchester City open their Premier League title defence next week, and similarly the likes of Bruno Zuculini are incredibly unlikely to feature.
But Manuel Pellegrini will still be bothered by his side's lack of cohesion and urgency.
The Chilean, usually quite reserved, was seen jabbing and prodding feverishly on the touchline during the first half as his side lacked urgency. It's not just the names that need to return to this City side, it's last season's fluency and desire.
Meanwhile for Arsenal, second string or not, it was a great way to finish pre-season with the three Germans yet to return and at least one new signing to come.
Four-four-f*****g-two


Formation men: Pellegrini got it wrong up against Wenger's side  
Manuel Pellegrini stuck with Mike Bassett's favourite formation for this game and it was a significant contributory factor in his side getting pummelled.
It is undoubtedly a useful shape, and one that will continue to see a revival this season with the parallel rise of the 3-5-2, but up against Arsenal's classic 4-2-3-1 there was simply too much for Fernando and Yaya Toure to deal with in that central area.
Wenger's men simply overran the game in midfield early on and the champions never got a foothold. Stevan Jovetic didn't particularly drop in and help out his floundering teammates while Edin Dzeko strolled around aimlessly in attack, and it was all too easy for the Gunners.




















Ndege nyingine yaanguka Iran nakuua abiria wote




qNdege  ya kampuni ya Taban Air imeripotiwa kuanguka katika makazi ya watu baada kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mehrabad Magharibi mwa mji wa Tehran nchini Iran.
Ndege hiyo inayojulikana kama Iran 141 ilitengezwa nchini Iran kwa teknologia ya Ukraine imepata ajari na kuua watu wote waliokuwepo kwenye hiyo ndege.
Kituo cha television cha taifa kimetangaza kuwa ndege hiyo ilikuwa na abiria 40 na uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea.
Iran imekabiliwa na ajali kama hizo katika siku za hivi karibuni kutokana na ndege zake zilizozeeka mbali na marekebisho mabaya inazozifanyia.

Promoter na Meneja mkubwa duniani abadiil jinsia na kuwa mama wa nyumbani



Dunia ni ya kipekee pia ni ngumu-kuzungumza kwamba aliyekuwa promoter na meneja  ambaye alifanya Lennox Lewis kuwa World Champion sasa anaishi kama mwanamke aitwaye Kellie


Kwa miongo mitatu, akijulikana kama pua ngumu(Hard nose)- Frank Maloney akitawala kama moja ya wafalme wa dunia, macho world of champion.

Maloney alikuwa promoter na meneja aliye fanikiwa kumuongoza Lennox Lewis kuwa muingereza wa kwanza kuwa bingwa wa dunia ambaye hakuwahi kupigwa  karibu karne kupita.

Mamilioni ya wapenzi wa ngumi wanamtazama kama sehemu ya kujifunza katika ulingo baada ya ushindi wake 1992.lakini sasa anafahamika kama mama wa nyumbani.


Lakini nje ya ulingo, Frank iliingia katika siri kubwa, na kuanza kutaabika katika mapambano ya yake huku akihofia angeweza kamwe asingewezakushinda.

KWA SASA.
Frank Maloney, 61, imegundulika kuwa anajiandaa kufanya mabadiliko ya jinsia na anaishi kama mwanamke aitwaye Kellie.

Katika  mahojiano, anaelezea jinsi alivyo anza kuisi utofauti katika mwili wake  kwa vile yeye alikuwa mtoto na  hatimaye alifanya uamuzi wake ambao anauita wa kijasiri na kuwa mwanamke.

Frank akiwa amewahi kuoa  mara mbili-na kufanikiwa kupata watoto wa tatu pia inaonyesha mke wa pili baada ya kupata taarifa juu ya mumewe akapata uchungu na kuamua kuachana huku hofu ya kuwepo kwa kuzorota kwa uwezo wake wa ndondi ukinukia. Lakini mwisho, kwa Kellie, anaishi kama mwanamke katika suala la maisha au kifo.
"Mimi nilizakiwa nikiwa tofauti na daima nilitambua kuwa nilikuwa mwanamke," alisema Frank  akaongeza kuwa sauti yake ngozi na hisia ndivyo vilimfanya awe tofauti.
"Siwezi kuendelea kuishi katika kivuli, ndio maana leo hii nimeamua kujitokeza hadharani.Kuishi na kitu moyoni kwa muda mrefu matokeo yake kinaweza kukuzulu na kukuletea matatizo,”alisema Maloney

KUHUSU WIVU

Katika mahojihano yaliokuwa yakiendelea Maloney alipata nafasi ya kuelezea wivu akiwa kama mwanamke na kusema"Kilicho kuwa kinanisumbua wakati nikiwa mtoto kwa kipo sawa kwa kuwa nina uwezo kama mwanamke(Female brain)baada ya kurekebiswha na madktari na kuwa na ubongo wa kike.Nilijua nilikuwa tofauti na watoto wengine lakini ni dakika chache nakuwa kama wao muda mrefu na kuwa na wivu wa kisichana,”alisema Maloney


Akijulikana kama Londoner Kellie akiwa na zaidi ya mwaka ndani ya kipindi cha mpito akijifunza kukabiliana na kuwa kama mwanamke.



Katika miaka miwili iliyopita Maloney alikuwa na siri kufanyiwa matibabu ya homoni, mamia ya masaa ya nywele kuondolewa electrolysis, kufundishwa kuwa na sauti ya kike na mtaalamu wa ushauri nasaha.
Miongozo ya  NHS katika hali  ya transsexual lazima kutumia miaka miwili kama unataka kuwa wakike kabla ya wao kukuruhusu kufanyiwa  upasuaji  wa  marekebisho.
 “Hisia na mavazi ya kike huko ndiko wanako fundisha “alisema Maloney na kuongeza kuwa hakutaka kuvaa mavazi ya kike lakini ilishindikana.
“Lakini sikuwa na uwezo wa kumwambia mtu yeyote katika ndondi,”alisema Maloney  akiongeza kuwa mtu ambaye alifanya nae kazi  Uingereza,Jumuiya ya Madola na Ulaya ndondi championi alikuwa ni Bingwa wa zamani wa dunia David Haye ikiwa katika level ya cruiserweight.
Kellie(Maloney) - ambaye alikuwa ameweza kumfanya  Lennox Lewis 1989-2001 kutambulika ulimwengu wa ndondi na baadae kuamua kukabiliana na ukweli na kujitambulisha kama yeye ni mwanamke.


Bunge la Katiba lawagawa wabunge wa CCM

mwigulu (1)Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza kumeguka baada ya baadhi ya wabunge wake ambao ni Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kuunga mkono kauli ya Naibu Katibu Mkuu wake, Mwigulu Nchemba.

Nchemba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, Jumanne iliyopita akichangia wakati wa mjadala wa mabadiliko ya kanuni, alilitaka Bunge Maalumu la Katiba lijitathmini kama lina ulazima wa kuendelea wakati hakuna uhakika wa kupatikana kwa theluthi mbili.

Alisema kitendo cha Bunge hilo kukaa kwa siku 84 bila uhakika wa kupatikana kwa theluthi mbili kwa pande zote mbili inayohitajika kupitisha Rasimu ya Katiba Mpya, hakiwezi kueleweka kwa Watanzania.

Nchemba alisema ni vyema kujua idadi ya wanaoshiriki awamu ya pili ya Bunge hilo ili kutoa uthibitisho  kimahesabu kama uamuzi wa kuendelea kwa Bunge unaweza kuwa na maana.


Jana Mwigulu Nchemba alizidi kusisitiza kauli aliyoitoa akisema ni msimamo wake binafsi kama mtoto wa maskini. Alisema anatambua jinsi walipa kodi watakavyoumia, rasimu hiyo itakapokwama kupita kutokana na kukosekana kwa theluthi mbili ya pande zote.

Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye  juzi alijibu akisema kauli ya Nchemba ni mtazamo wake binafsi na hakuongea kama kiongozi wa chama hicho.

Lakini jana wabunge mbalimbali wa CCM walijitokeza hadharani wakisema wanaunga mkono kauli ya Nchemba ili hesabu ijulikane badala ya kuendelea kutafuna fedha za wananchi bila tija.

Saturday, 9 August 2014

Hali ya sintofahamu inayoendelea katika jengo la Machinga Complex lililoko katika Manispaa ya Ilala



Takribani  miaka sita sasa toka jengo la Machinga Complex likabidhiwe kwa mamlaka husika litumike kama eneo rasmi la biashara lakini bado viongozi wenye dhamana  ya jengo hilo wanasita kuonyesha  nia ya dhati katika kulifanya jengo hilo liwe na tija kwa wafanya biashara wa eneo hilo.
Hali hiyo, inapelekea  wafanya biashara wengi kutokuthamini kuweko kwa jengo hilo na kuona halina  msaada kwao, kutokana na madai ya kuwepo kwa mapungufu makubwa katika maeneo ya jengo hilo ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa miundo mbinu mibovu, kukosekana kwa lift na kutokuweko kwa  kituo cha mabasi ambacho kitasaidia  kuwepo kwa wateja wanao toka maeneo mbalimbali jijini.
Mwenyekiti wa wanyabiashara katika jengo hilo, Abubakari Rakesh, anasema jengo limekosa miundombinu ambayo ni muhimu kwa ustawi wa wanyabiashara  na kukosekana kwa kituo cha mabasi ambacho kingekuwa chachu ya kupatikana kwa wateja.
“Miundombinu ya jengo si mizuri kwa kukosa vitu muhimu kama vile lift,kituo cha mabasi na mazingira mazuri ya kufanyia biashara ndio maana utaona wafanyabiashara wengi bado wapo soko la Karume kwakuwa pale kuna kituo cha mabasi na kuna wateja wengi kwa hiyo ni vigumu kuwashawishi kuja eneo amabalo kwao halina tija,” anafafanua Rakeshi
Rakeshi anasema hali hiyo imepelekea kuwaomba halmashauri ya jiji na manispaa ya Ilala iwasaidie katika kutatua kero hizo za muda mrefu kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya jengo lakini mpaka sasa hawajaonesha nia ya dhati katika kutatua madai hayo ambayo yanatoka kwa wafanyabiashara.
Anasema mpaka sasa ni asilimia 30 ambazo zinaonesha muelekeo wa mafanikio ya jengo toka limekabidhiwa kwa mamlaka husika japo kuwa tunapiga hatua katika kushawishi lakini bado zinatakiwa jitihada za makusudi katika kuhakikisha madai ya wafanyabiashara yana sikilizwa na kupatiwa ufumbuzi wa kina.
Katika kukikisha wanatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazopatikana katika jengo hilo, Rakesh anasema Agosti 31 mwaka jana walikutana na kamati ya (MILADI TAMISEMI) Dodoma,chini ya Mwenyekiti  Dk Hamisi Kigwangala.
“Katika kueleza kamati matatizo yanayotukabili ikiwa pamoja na jengo kukosa lift , kituo cha mabasi,na uwepo kituo cha kuoshea magari mbele ya jengo licha ya kupelekea  usumbufu kwa wateja pia inachangia muonekano mbaya wa jengo, bado mpaka sasa hakuna matokeo yeyote kutoka katika kamati hiyo ambayo yangetoa  ufumbuzi, japokuwa  walituahidi wangetupatia ufumbuzi wa suala hilo mapema,” alisema Rakeshi.
Naye Mwenyekiti Msaidizi, Gerald B.Mpagama,anasema madai ya wafanyabiashara yanagusa  maslahi binafsi ya viongozi walio pewa dhamana,inapelekea  madai hayo yenye msingi kutosikilizwa na kutatuliwa na viongozi hao jambo ambalo linadhohofisha  makusudio na malengo ya serikali katika kufanikisha kuwepo kwa jengo hilo.
“Viongozi wa Halmashauri ya jiji na Manispaa ya Ilala kutokana na maslahi yao binafsi wamekuwa chanzo cha kuwako kwa matatizo haya kwa muda mrefu na kupelekea kudhoofisha kupatikana kwa ufumbuzi wa  matatizo wakati wakijua fika kuwa kuna hasara kubwa inayo patikana kutokana na malengo na makusudio ya kuwepo kwa jengo kutotimia kama ilivyotarajiwa ,”anasema Mpagama.
Mpagama anasema kimsingi Rais Kikwete alitimiza ahadi yake na kulikabidhi jengo tangu 2009, muda wote huo mamlaka husika wameshindwa kusimamia majukumu yao na kusababisha hasara kubwa kutokana na wafanyabiashara wengi bado hawaja shawishika kutokana na kutokuwepo na miundombinu itakayo wavutia wateja.
“Hii sio (mall) kama Mlimani city, kama viongozi wanashindwa kufahamu kuwa pesa nyingi zimetumika kujenga jengo hili na mpaka sasa malengo hayajafikia hata robo,wao baada ya kutatua matatizo hili tufikie malengo,wanadharau na kufikilia ubinafsi na ukiangalia kwa kina Meya wa manispaa ya Ilala (Jeri Slaa) ndio hajafanya  lolote na kashindwa kusimamia kazi yake kwa maslahi ya umma,badala yake yeye anaendeleza  maslahi binafsi, ”alilalamika  Mpagama.
Anasema zipo baadhi ya changamoto zinazo tokana na utoro wa wanyabiashara ambao wanakuwa na vizimba ambavyo hawafanyii biashara bado tunaendelea kufanyia kazi na katika kukabiliana na hilo tumeamua kuchukua vizimba vyote kwa wafanyabiashara wote wasio na sifa na kuwapa wengine ambao wenye sifa tunazo taka.
“kufungwa kwa vizimba vingi inasababiswa na kuwepo kwa utoro na kupoteza sifa kwa wafanyabiashara wengi wenye vizimba, kutokana na hali hiyo tumeamua  kuchukua vizimba vyote kwa wafanyabiashara walio poteza sifa na wasiokuwa tayari katika maendeleo ya jengo hili  ili tuwapatie wenye sifa za kufanya biashara, ”anafafanua Mpagama.
Katika jitihada za kumtafuta Meya wa jiji la Dar es salaam, Didas Masabuli, ili kujua kwamba ni namna gani ameweza kutafuta ufumbuzi wa  tatizo hilo la muda mrefu, Meya wa jiji alidai kuwa hajui madai hayo na kuelekeza labda mkurugenzi wa jiji angeweza kutambua madai hayo.
“Ningeshauri atafutwe Mgurugenzi wa jiji labda  yeye ndio mwenye data kamili ambazo zitamuezesha kuongelea suala hilo kwa kina,lakini mimi siwezi kuliongelea hilo kwa kuwa hawaku leta madai yao  kwangu , hata hivyo  madai  yao siyatambui  ndio maana nimeshauri  atafutwe mkurugenzi wa jiji ili aliongelee suala hilo, ”anasema Masabuli.
Alipotafutwa Mkurugenzi wa jiji naye alimtaka mwandishi kumtafuta kiongozi wa jengo kwa kuwa hayuko tayari kulizungumzia suala hilo.
Katika kikao cha kamati (MILADI TAMISEMI), ambacho kilikuwa chini ya mwenyekiti Dk Hamisi kigwangala na waziri Hawa Ghasia, kilichofanyika Agosti 31 mwaka jana mjini Dodoma, kwa mujibu wa mwenyekiti wa wanyabiashara wa Machinga  complex kinaonyesha kuwa baadhi ya viongozi waliokuwepo pamoja na  Meya wa jiji la Dar es salaam Didas Masabuli.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Rakesh, katika kikao na kamati hiyo alipata nafasi ya  kuelezea madai yao mbele ya kamati hiyo pia wakiwemo viongozi  wa jiji na kudai kwamba wange ya shuhulikia madai hayo lakini mpaka sasa hapaja kuwapo matokeo yeyote amabayo yangekuwa ni matokeo mazuri ya kikao hicho.
“Nasikitika sana kwa Meya wa jiji anaposema hayatambui madai yetu, katika kikao ambacho tulikutana na kamati ya (MILADI TAMISEMI) Dodoma,chini ya mwenyekiti  Dk Hamisi Kigwangala, tukieleza madai yetu nayeye (Didas Masabuli), alikuwapo kwenye  kikao hicho,na haya madai yapo kwa kipindi cha miaka sita sasa,sidhani kama kuna kiongozi mwenye dhamana na hili jengo anaweza kusema hajui madai ya wafanya biashara kama anavyodai yeye (Masaburi), kwamba hayajui madai yetu, ” anasema Rakesh.
Ikumbukwe kwamba jengo hilo lilijengwa kwa mkopo wa NSSF na likakabidhiwa kwa viongozi wa Halmashauri ya jiji  na manispaa ya Ilala miaka sita iliyopita lakini mpaka sasa shughuli katika jengo hilo