Showing posts with label Sports Tanzania. Show all posts
Showing posts with label Sports Tanzania. Show all posts

Wednesday, 6 August 2014

Yanga yaijibu CECAFA baada ya kuondolewa Kagame Cup


Siku moja baada ya Shirikisho la vyama vya soka Afrika mashariki na kati CECAFA kuiondoa klabu ya Yanga kwenye michuano ya Kagame Cup itakayofanyika Rwanda, leo hii uongozi wa klabu ya Yanga umetoa maelezo juu ya kuondolewa kwenye michuano hiyo.
Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA.
“Baada ya kudhibitisha kushiriki michuano hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya wachezaji na viongozi ambao watasafiri kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano hiyo ili waweze kuandaa tiketi za ndege na sehemu ya malazi kitu ambacho tulitimiza” alisema Beno.
Lakini katika hali ya kushangaza jana tulipokea barua kutoka TFF ikisema CECAFA imetuondoa kwenye mashindano hayo kwa kushindwa kukidhi vigezo na kuiteua timu ya Azam kuchukua nafasi yetu “aliongeza Beno.”
Kanuni za CECAFA zipo wazi kuwa wachezaji wanaopaswa kushiriki michuano hiyo ni lazima wawe na leseni za kucheza mpira kutoka kwa chama husika, jambo ambalo ambalo orodha tuliyowapelekea wachezaji wote wataichezea Yanga msimu huu wa 2014/2015.
Kocha Marcio Maximo alianza maandalizi ya kikosi ambacho kingekwenda kushiriki michuano hiyo ambayo ilipaswa kuanza ijumaa tarehe 8/8/2014 kwa Yanga kufungua dimba la wenyeji timu ya Rayon FC .
Kikosi ambacho kocha mkuu alikichagua kwenda kwenye michuano ya Kagame kilikua na jumla ya wachezaji 20, 15 wakiwa kutoka timu ya kikosi cha wakubwa na wachezaji watano wakitoka kikosi cha pili U20 chini ya kocha Leonado Neiva ambaye amekua na wachezaji hao kwa takribani mwezi mmoja.
Lakini walichokiamua CECAFA ni kuiondoa klabu ya Yanga na kuipa nafasi timu nyingine kwa kusema kikosi kilichopelekwa hawakubaliani nacho na hata kocha mkuu Marcio Maximo haendi, hao ndo tulipojua ya kuwa wanataka majina ya watu na sio timu.
Zifuatazo ni sababu za Kiufundi ambazo Yanga ilizipelekea CECAFA kuhusu kikosi hicho kutojumuisha wachezaji wa timu za Taifa.
a) Ripoti ya kocha aliyeondoka Yanga msimu uliopita Hans ilitoa maelekezo ya kupunguza wachezaji tisa (9) na wachezaji wawili kujiunga na klabu ya Azam hivyo kufanya kikosi kupungua wachezaji 11 kutoka katika idadi ya wachezaji 30 wa msimu uliopita.
b) Wachezaji 10 wa Yanga wamekuwa na majukumu ya timu za Taifa za Tanzania (Taifa Stars), Rwanda na Uganda tangu Aprili 19, 2014 mpaka mwanzoni mwa Agosti, takribani miezi mitatu wamekuwa kambini bila kupata muda wa kupumzika.
c)  Benchi la Ufundi la Yanga ni jipya kuanzia kocha mkuu Maximo na wasaidizi wake watatu Leonardo Neiva, Salavatory Edwarda na Shadrack Nsajigwa hivyo wanahitaji muda wa kuwajua wachezaji waliokuwa kwenye timu ya Taifa ndo maana hawakuwajumuisha kwenye kikosi cha kwenda Kigali Rwanda.
d)  Baadhi ya wachezaji wanahitaji Vibali vya kufanyia kazi nchini, uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili waweza kushiriki michuano ya Kagame, na moja ya kanuni za CECAFA mchezaji anayeshiriki mashindano hayo ni lazima awe na leseni ya kucheza mpira kwa ligi ya ndani.
e) Katika wachezaji 20 waliochaguliwa kushiriki michuano ya Kagame, wachezaji 6 wamepandishwa moja moja katika kikosi cha wakubwa msimu huu hivyo kufanya idadi ya wachezaji wa U20 kuwa watano tu.
f) Wachezaji walikokuwa kambini Taifa Stars kwa takribani miezi mitatu bila ya kupumzika, daktari alipendekeza wapate japo siku kumi na nne (14) za kupumzika ili miili yao iweze kupoa na kuanza upya tena maandalizi ya msimu mpya.
g) Yangga tunaamini hakuna mtu yoyote zaidi ya Kocha Mkuu anayeweza kutupangia kikosi cha kwanza, sababu yeye ndio anayekaa na wachezaji mda wote na kujua ubora wa wachezaji wake

Thursday, 17 July 2014

Je, TZ kufuta uteja katika mashindano ya Jumiya ya Madola mjini Glasgow mwaka huu?

Katibu Mkuu wa kamati ya Olympiki ya Tanzania Filbert Bayi ametangaza kikosi cha wanamichezo 37 na maafisa 10 watakaoiwakilisha Tanzania kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow, Scotland, kuanzia Julai tarehe 23.
Mkuu wa kikosi hicho ni mkurugenzi wa michezo nchini Tanzania Leonard Thadeo.
Tangu michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka wa 2006 Tanzania iliposhinda medali mbili - dhahabu kupitia Samson Ramadhan na shaba ya Fabian Joseph Naali - Tanzania haijashinda medali tena kwenye michezo hii.
Je, mwaka huu unaona Tanzania itazoa dhahabu nyingi zaidi mjini Glasgow? toa maoni yako katika ukurasa wetu wa Facebook:issaadam21@yahoo.com

Tuesday, 15 July 2014

Tanzania yapata semina yakuzuia kupanga matokeo


Timu ya taifa ya Tanzania
Kituo cha Kimataifa cha Ulinzi wa michezo (International Centre for Sport Security) wiki hii kitatoa elimu kuhusu kupiga vita upangaji wa matokeo kwa wanamichezo vijana wa kiafrika.
Kama njia mojawapo ya Kituo hicho kubeba mzigo wa kuwaelimisha wachezaji vijana kuhusu madhara ya kupanga matokeo , Stuart Page Mkurugenzi Mkakati na maendeleo ya sera wa Kituo hicho na Jake Marsh, Mchunguzi wa kituo hicho , wataongoza warsha ya siku tatu itakayohusu namna ya kurejesha hadhi kupiga vita upangaji matokeo kwa wachezaji vijana na maafisa watakaoongozwa na viongozi wa chama cha soka Tanzania, kikiwemo Chama cha Soka Tanzania, mradi wa Kampuni ya Symbion/Sunderland AFC ambayo ni kampuni binafsi ya kwanza barani Afrika inayomiliki chuo cha soka pamoja na chuo cha michezo cha watoto wa mitaani kilichopo Tanzania.
Taarifa zaidi
  • michezo
Warsha hiyo ina lengo la kufundisha wanamichezo vijana wenye umri kati ya miaka 12 hadi 18 wanaotoka katika vyuo vya michezo pamoja na watoto wa Tanzania wanaoishi maeneo hatarishi.
Warsha hiyo itaanza kwa kuwafundisha wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania walio chini ya Umri wa miaka 17 katika uwanja Karume mjini Dar es Salaam nchini Tanzania.
Wachezaji watakaohudhuria semina hiyo watajifunza mada mbali mbali ikiwemo namna ya kuzuia kupanga matokeo na kuinua vipaji vya wachezaji vijana, mbinu za kubaini, kuzuia na kuripoti mpango hiyo na namna ya kuonya kuhusu mipango hiyo hatari ya kupanga matokeo.
Stuart Page wa Kituo hicho cha Kimataifa anasema " Elimu na Kinga ndio msingi wa Kituo hicho kuondoa matatizo ya upangaji wa matokeo na hasa wanariadha ndio msingi wa mkakati wa kituo hicho."

Monday, 14 July 2014

Mwinyi, Mkapa, Jakaya kutunukiwa tuzo Agosti 30

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kupewa tuzo na Kituo cha Michezo cha Sinza cha jijini Dar es Salaam (SSSCC), katika kumbua mchango wake katika maendeleo ya sekta ya michezo nchini.
Mbali ya Kikwete, wengine watakaopewa tuzo katika hafla hiyo ya Agosti 30, ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili na Tatu; Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa na wengineo kutokana na mchango wao.
Tuzo hizo zilizondaliwa na kituo hicho kwa kushirikiana na Chama cha michezo, Utamaduni na Sanaa kwa Watanzania Wote (TAFISA), zitafanyika siku katika Hotel ya Delux Sinza.


Kwa mujibu wa Mratibu wa hafla hiyo, Kadatta Kaswella, alisema lengo ni kuwapongeza viongozi hao kama ishara ya kutambua juhudi zao katika maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Viongozi wengine katika tuzo hizo ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Afrika Mashariki, Samweli Sitta, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuri, Waziri wa Aridhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi, Pfof Anna Tibaijuka.
Wengine ni Juma Nkamia (Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo), Kassim Ally Mtawa (Msaidizi Mahususi wa Rais), IGP Evarist Mangu (Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania) na Abdulrahman Kaniki (Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi).
Kuhusu Mkapa, alisema ni jitihada zake za kuwaachia Watanzania Uwanja wa Taifa ambao unalisaidia Taifa katika mashindano  huku Waziri Nkamia akipongezwa kwa kuteuliwa kwake, hivyo ni busara kuwapongeza watu wakiwa hai.


Aliongeza, siku hiyo ya hafla mgeni rasmi atakuwa Waziri Dk. Mwankyembe huku hafla hiyo ikipambwa na burudani murua.