Showing posts with label Feature. Show all posts
Showing posts with label Feature. Show all posts

Sunday, 10 August 2014

Promoter na Meneja mkubwa duniani abadiil jinsia na kuwa mama wa nyumbani



Dunia ni ya kipekee pia ni ngumu-kuzungumza kwamba aliyekuwa promoter na meneja  ambaye alifanya Lennox Lewis kuwa World Champion sasa anaishi kama mwanamke aitwaye Kellie


Kwa miongo mitatu, akijulikana kama pua ngumu(Hard nose)- Frank Maloney akitawala kama moja ya wafalme wa dunia, macho world of champion.

Maloney alikuwa promoter na meneja aliye fanikiwa kumuongoza Lennox Lewis kuwa muingereza wa kwanza kuwa bingwa wa dunia ambaye hakuwahi kupigwa  karibu karne kupita.

Mamilioni ya wapenzi wa ngumi wanamtazama kama sehemu ya kujifunza katika ulingo baada ya ushindi wake 1992.lakini sasa anafahamika kama mama wa nyumbani.


Lakini nje ya ulingo, Frank iliingia katika siri kubwa, na kuanza kutaabika katika mapambano ya yake huku akihofia angeweza kamwe asingewezakushinda.

KWA SASA.
Frank Maloney, 61, imegundulika kuwa anajiandaa kufanya mabadiliko ya jinsia na anaishi kama mwanamke aitwaye Kellie.

Katika  mahojiano, anaelezea jinsi alivyo anza kuisi utofauti katika mwili wake  kwa vile yeye alikuwa mtoto na  hatimaye alifanya uamuzi wake ambao anauita wa kijasiri na kuwa mwanamke.

Frank akiwa amewahi kuoa  mara mbili-na kufanikiwa kupata watoto wa tatu pia inaonyesha mke wa pili baada ya kupata taarifa juu ya mumewe akapata uchungu na kuamua kuachana huku hofu ya kuwepo kwa kuzorota kwa uwezo wake wa ndondi ukinukia. Lakini mwisho, kwa Kellie, anaishi kama mwanamke katika suala la maisha au kifo.
"Mimi nilizakiwa nikiwa tofauti na daima nilitambua kuwa nilikuwa mwanamke," alisema Frank  akaongeza kuwa sauti yake ngozi na hisia ndivyo vilimfanya awe tofauti.
"Siwezi kuendelea kuishi katika kivuli, ndio maana leo hii nimeamua kujitokeza hadharani.Kuishi na kitu moyoni kwa muda mrefu matokeo yake kinaweza kukuzulu na kukuletea matatizo,”alisema Maloney

KUHUSU WIVU

Katika mahojihano yaliokuwa yakiendelea Maloney alipata nafasi ya kuelezea wivu akiwa kama mwanamke na kusema"Kilicho kuwa kinanisumbua wakati nikiwa mtoto kwa kipo sawa kwa kuwa nina uwezo kama mwanamke(Female brain)baada ya kurekebiswha na madktari na kuwa na ubongo wa kike.Nilijua nilikuwa tofauti na watoto wengine lakini ni dakika chache nakuwa kama wao muda mrefu na kuwa na wivu wa kisichana,”alisema Maloney


Akijulikana kama Londoner Kellie akiwa na zaidi ya mwaka ndani ya kipindi cha mpito akijifunza kukabiliana na kuwa kama mwanamke.



Katika miaka miwili iliyopita Maloney alikuwa na siri kufanyiwa matibabu ya homoni, mamia ya masaa ya nywele kuondolewa electrolysis, kufundishwa kuwa na sauti ya kike na mtaalamu wa ushauri nasaha.
Miongozo ya  NHS katika hali  ya transsexual lazima kutumia miaka miwili kama unataka kuwa wakike kabla ya wao kukuruhusu kufanyiwa  upasuaji  wa  marekebisho.
 “Hisia na mavazi ya kike huko ndiko wanako fundisha “alisema Maloney na kuongeza kuwa hakutaka kuvaa mavazi ya kike lakini ilishindikana.
“Lakini sikuwa na uwezo wa kumwambia mtu yeyote katika ndondi,”alisema Maloney  akiongeza kuwa mtu ambaye alifanya nae kazi  Uingereza,Jumuiya ya Madola na Ulaya ndondi championi alikuwa ni Bingwa wa zamani wa dunia David Haye ikiwa katika level ya cruiserweight.
Kellie(Maloney) - ambaye alikuwa ameweza kumfanya  Lennox Lewis 1989-2001 kutambulika ulimwengu wa ndondi na baadae kuamua kukabiliana na ukweli na kujitambulisha kama yeye ni mwanamke.


Saturday, 9 August 2014

Hali ya sintofahamu inayoendelea katika jengo la Machinga Complex lililoko katika Manispaa ya Ilala



Takribani  miaka sita sasa toka jengo la Machinga Complex likabidhiwe kwa mamlaka husika litumike kama eneo rasmi la biashara lakini bado viongozi wenye dhamana  ya jengo hilo wanasita kuonyesha  nia ya dhati katika kulifanya jengo hilo liwe na tija kwa wafanya biashara wa eneo hilo.
Hali hiyo, inapelekea  wafanya biashara wengi kutokuthamini kuweko kwa jengo hilo na kuona halina  msaada kwao, kutokana na madai ya kuwepo kwa mapungufu makubwa katika maeneo ya jengo hilo ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa miundo mbinu mibovu, kukosekana kwa lift na kutokuweko kwa  kituo cha mabasi ambacho kitasaidia  kuwepo kwa wateja wanao toka maeneo mbalimbali jijini.
Mwenyekiti wa wanyabiashara katika jengo hilo, Abubakari Rakesh, anasema jengo limekosa miundombinu ambayo ni muhimu kwa ustawi wa wanyabiashara  na kukosekana kwa kituo cha mabasi ambacho kingekuwa chachu ya kupatikana kwa wateja.
“Miundombinu ya jengo si mizuri kwa kukosa vitu muhimu kama vile lift,kituo cha mabasi na mazingira mazuri ya kufanyia biashara ndio maana utaona wafanyabiashara wengi bado wapo soko la Karume kwakuwa pale kuna kituo cha mabasi na kuna wateja wengi kwa hiyo ni vigumu kuwashawishi kuja eneo amabalo kwao halina tija,” anafafanua Rakeshi
Rakeshi anasema hali hiyo imepelekea kuwaomba halmashauri ya jiji na manispaa ya Ilala iwasaidie katika kutatua kero hizo za muda mrefu kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya jengo lakini mpaka sasa hawajaonesha nia ya dhati katika kutatua madai hayo ambayo yanatoka kwa wafanyabiashara.
Anasema mpaka sasa ni asilimia 30 ambazo zinaonesha muelekeo wa mafanikio ya jengo toka limekabidhiwa kwa mamlaka husika japo kuwa tunapiga hatua katika kushawishi lakini bado zinatakiwa jitihada za makusudi katika kuhakikisha madai ya wafanyabiashara yana sikilizwa na kupatiwa ufumbuzi wa kina.
Katika kukikisha wanatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazopatikana katika jengo hilo, Rakesh anasema Agosti 31 mwaka jana walikutana na kamati ya (MILADI TAMISEMI) Dodoma,chini ya Mwenyekiti  Dk Hamisi Kigwangala.
“Katika kueleza kamati matatizo yanayotukabili ikiwa pamoja na jengo kukosa lift , kituo cha mabasi,na uwepo kituo cha kuoshea magari mbele ya jengo licha ya kupelekea  usumbufu kwa wateja pia inachangia muonekano mbaya wa jengo, bado mpaka sasa hakuna matokeo yeyote kutoka katika kamati hiyo ambayo yangetoa  ufumbuzi, japokuwa  walituahidi wangetupatia ufumbuzi wa suala hilo mapema,” alisema Rakeshi.
Naye Mwenyekiti Msaidizi, Gerald B.Mpagama,anasema madai ya wafanyabiashara yanagusa  maslahi binafsi ya viongozi walio pewa dhamana,inapelekea  madai hayo yenye msingi kutosikilizwa na kutatuliwa na viongozi hao jambo ambalo linadhohofisha  makusudio na malengo ya serikali katika kufanikisha kuwepo kwa jengo hilo.
“Viongozi wa Halmashauri ya jiji na Manispaa ya Ilala kutokana na maslahi yao binafsi wamekuwa chanzo cha kuwako kwa matatizo haya kwa muda mrefu na kupelekea kudhoofisha kupatikana kwa ufumbuzi wa  matatizo wakati wakijua fika kuwa kuna hasara kubwa inayo patikana kutokana na malengo na makusudio ya kuwepo kwa jengo kutotimia kama ilivyotarajiwa ,”anasema Mpagama.
Mpagama anasema kimsingi Rais Kikwete alitimiza ahadi yake na kulikabidhi jengo tangu 2009, muda wote huo mamlaka husika wameshindwa kusimamia majukumu yao na kusababisha hasara kubwa kutokana na wafanyabiashara wengi bado hawaja shawishika kutokana na kutokuwepo na miundombinu itakayo wavutia wateja.
“Hii sio (mall) kama Mlimani city, kama viongozi wanashindwa kufahamu kuwa pesa nyingi zimetumika kujenga jengo hili na mpaka sasa malengo hayajafikia hata robo,wao baada ya kutatua matatizo hili tufikie malengo,wanadharau na kufikilia ubinafsi na ukiangalia kwa kina Meya wa manispaa ya Ilala (Jeri Slaa) ndio hajafanya  lolote na kashindwa kusimamia kazi yake kwa maslahi ya umma,badala yake yeye anaendeleza  maslahi binafsi, ”alilalamika  Mpagama.
Anasema zipo baadhi ya changamoto zinazo tokana na utoro wa wanyabiashara ambao wanakuwa na vizimba ambavyo hawafanyii biashara bado tunaendelea kufanyia kazi na katika kukabiliana na hilo tumeamua kuchukua vizimba vyote kwa wafanyabiashara wote wasio na sifa na kuwapa wengine ambao wenye sifa tunazo taka.
“kufungwa kwa vizimba vingi inasababiswa na kuwepo kwa utoro na kupoteza sifa kwa wafanyabiashara wengi wenye vizimba, kutokana na hali hiyo tumeamua  kuchukua vizimba vyote kwa wafanyabiashara walio poteza sifa na wasiokuwa tayari katika maendeleo ya jengo hili  ili tuwapatie wenye sifa za kufanya biashara, ”anafafanua Mpagama.
Katika jitihada za kumtafuta Meya wa jiji la Dar es salaam, Didas Masabuli, ili kujua kwamba ni namna gani ameweza kutafuta ufumbuzi wa  tatizo hilo la muda mrefu, Meya wa jiji alidai kuwa hajui madai hayo na kuelekeza labda mkurugenzi wa jiji angeweza kutambua madai hayo.
“Ningeshauri atafutwe Mgurugenzi wa jiji labda  yeye ndio mwenye data kamili ambazo zitamuezesha kuongelea suala hilo kwa kina,lakini mimi siwezi kuliongelea hilo kwa kuwa hawaku leta madai yao  kwangu , hata hivyo  madai  yao siyatambui  ndio maana nimeshauri  atafutwe mkurugenzi wa jiji ili aliongelee suala hilo, ”anasema Masabuli.
Alipotafutwa Mkurugenzi wa jiji naye alimtaka mwandishi kumtafuta kiongozi wa jengo kwa kuwa hayuko tayari kulizungumzia suala hilo.
Katika kikao cha kamati (MILADI TAMISEMI), ambacho kilikuwa chini ya mwenyekiti Dk Hamisi kigwangala na waziri Hawa Ghasia, kilichofanyika Agosti 31 mwaka jana mjini Dodoma, kwa mujibu wa mwenyekiti wa wanyabiashara wa Machinga  complex kinaonyesha kuwa baadhi ya viongozi waliokuwepo pamoja na  Meya wa jiji la Dar es salaam Didas Masabuli.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Rakesh, katika kikao na kamati hiyo alipata nafasi ya  kuelezea madai yao mbele ya kamati hiyo pia wakiwemo viongozi  wa jiji na kudai kwamba wange ya shuhulikia madai hayo lakini mpaka sasa hapaja kuwapo matokeo yeyote amabayo yangekuwa ni matokeo mazuri ya kikao hicho.
“Nasikitika sana kwa Meya wa jiji anaposema hayatambui madai yetu, katika kikao ambacho tulikutana na kamati ya (MILADI TAMISEMI) Dodoma,chini ya mwenyekiti  Dk Hamisi Kigwangala, tukieleza madai yetu nayeye (Didas Masabuli), alikuwapo kwenye  kikao hicho,na haya madai yapo kwa kipindi cha miaka sita sasa,sidhani kama kuna kiongozi mwenye dhamana na hili jengo anaweza kusema hajui madai ya wafanya biashara kama anavyodai yeye (Masaburi), kwamba hayajui madai yetu, ” anasema Rakesh.
Ikumbukwe kwamba jengo hilo lilijengwa kwa mkopo wa NSSF na likakabidhiwa kwa viongozi wa Halmashauri ya jiji  na manispaa ya Ilala miaka sita iliyopita lakini mpaka sasa shughuli katika jengo hilo

Ajira za majumbani kichocheo cha ukatili wa kijnsia




MATUKIO ya ukatili wa kijinsia ni moja ya mambo yanayorudisha nyuma harakati za kumkomboa mtoto wa kike katika ukatili wa kijinsia.
Zipo njia nyingi zinazotumika kuendesha matukio ya ukatili wa kijnsia ikiwemo ajira za majumbani, ambazo kwa asilimia kubwa zinaendelea kuchochea suala hilo huku walengwa wakiwa hawajui sehemu ya kwenda haki zao.
Baadhi ya watu katika jamii ambao wamekuwa si waaminifu wamekuwa wakiitumia dhana ya ajira za majumbani kuendesha vitendo vya kijinsia.
Watu hao mara nyingi katika kutekeleza uovu wao wamekuwa wakienda vijijini na kuchukua wasichana wadogo kwa kuwarubuni kuwaleta Dar esSalaam kwa ajili ya kufanya kazi za ndani huku wakijua si kweli.
“Katika mradi wetu tulibaini kuwa wapo watu ambao wanakwenda vijijini wanachukua wasichana na kuwaahidi kuwa wanawaleta kwa ajili ya kazi za ndani, lakini baadaye inakuwa tofauti, kuna mfano mmoja ambao tumeuona Bagamoyo ambako tunaendesha mradi huu pia, msichana alichukuliwa kutoka Ludewa kuwa analetwa Dar es Salaam kwa ajili ya kazi za ndani, lakini baadaye kumbe huyo mtu alikuwa na lengo jingine kichwani mwake.
“Mtu huyo aliyejifanya ni msamaria mwema kumbe lengo lake alitaka kuishi naye kama mke na mume, binti yule mdogo mwenye umri wa miaka 16 hakukubali kitendo, siku moja waelimishaji rika ambao tuliwapa mafunzo maalum walipata taarifa juu ya jambo lile na walikwenda hadi katika nyumba ya yule mhusika aliyejifanya msamaria mwema na kumchukua kwa ajili ya kumpatia msaada,” anasema Dk. Makula.
Anasema baada ya kuhojiwa msichana huyo alieleza jinsi alivyochukuliwa na ahadi aliyopewa lakini alijikuta Bagamoyo akitakiwa kuwa mke jambo ambalo hakukubaliana nalo.
 “baada ya kupata maelezo yake walimsaidia lakini pia walimpeleka  kituo cha polisi na kufungua jalada na baada ya taarifa zile kumfikia mhusika alikimbia lakini hadi sasa hivi anatafutwa kwa ajili ya kuchukulia hatua za kisheria,” anasema Dk Makula.
Anasema kupitia mradi wao wa kupinga ukatili wa kijinsia na mapambano ya Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (GBV/HIV ambao unafanyika katika kata kumi na sita Wilayani Bagamoyo wameweza kufanikiwa kufanya kazi kwa ukaribu na wanajamii ambako wameweza kuibua matukio makubwa.
Dk.Makula anasema baada ya kuwapata wasichana waliokumbana na masuala ya ukatili wa kijinsia huanza kuwahoji, kufikisha mashauri yao kwa wenyeviti wa serikali za mitaa na baadaye Polisi kwa ajili ya kufungua mashitaka.
“Hawa wana mawasiliano jamii tumewapa elimu ya kutosha kuweza kupata taarifa sahihi kwa kila mtu wanayesikia amepata matatizo ya ukatili au masuala ya Ukimwi, tunazungumza nao kwanza wajue njia gani watanatakiwa kuzipitia kuweza kupata haki zao, pili tunawaelekeza namna ya kufuatia kupata hizo haki na sisi wenyewe tukiwasaidia,tunaendesha programu hii kwa msaada wa Mfuko wa dharura wa Kimataifa wa kusaidia mapambano dhidi ya Ukimwi ( RFE).
Anasema wameweza kutoa mafunzo kwa wanamawasiliano jamii ambao kwa elimu waliyopata wameweza kuleta mabadiliko katika jamii wanayoishi.
“Kumekuwa na mwamko kwamba watu wanaweza kutoa taarifa za matatizo wanayokumbana nayo katika jamii,sasa hivi wanawake au wasichana wakifanyiwa masuala ya ukatili wa kijinsia wanakuwa tayari kutoa taarifa tofauti na mwanzoni, mwako umekuwa mkubwa tofauti na mwanzoni,” anasema Dk.Makula.
Anasema baadhio ya watu katika jamii wamekuwa si wa kweli kwani wamekuwa wakiwachukua wasichana vijijini kwa ahadi za kuwapatia kazi za ndani kitu ambacho si kweli.
“Sasa hivi baada ya elimu kuwafikia vizuri imekuwa rahisi, kwasababu hawa wasichana wanaofanyia ukatili kwa dhana kwamba wanakuja kutafutiwa kazi za ndani ni wengi, jamii imekuwa ikibadilisha mbinu kila wakati, lakini sasa hali inaanza kuabdilika kwamba inapotokea mtu anakumbana na jambo lile basi wanakwenda kutoa taarifa.
Suala la ukatili wa kijinsia limekuwa likikuwa kila siku kutokana na kadri jamii inavyobadilisha mfumo wa maisha.
Imekuwa kawaida kwa watu kutumia vigezo vya kutafuta wafanyakazi wa ndani lakini baadaye wengi hutelekeza katiia maeneo mbalimbali baadaya kufanyiwa ukatili wa kijinsia ikiwemo kubakwa na wakati mwingine kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi.
Jamii kwa kushirikiana na serikali imekuwa ikipigia kelele suala hili lakini mara nyingi wasichana hao ambao ni wahusika wakuu wamekuwa hawana taarifa sahihi za wapi waende kutoa taarifa kwa ajili ya kupata msaada wa kisheria.

Mwisho




Thursday, 7 August 2014

Ten things that always happen in soaps but never in real life

WHENEVER I sit down to watch my favourite soap (Coronation Street) I find myself shouting at the TV because there are so many things happening that are simply unbelievable.


10 things that always happen in soaps but never in real lifeCome on Deirdre crack a tear, you just told him his son was in jail! [ITV]
Yes I know it's not real life but so many things in soaps simply don't wash.
I was keen to catch up with Corrie this week as Ken Barlow returned. He's been "away" - ostensibly in Canada looking after a sick relative - but actually the actor who plays him, William Roache (soap's longest running actor and character), was on trial for historic sex offences. He has now been cleared and returned on Monday, flinging open the door of number 1 Coronation Street and surprising his extremely evasive wife Deirdre, who was harbouring A SECRET.
Ken's return took the ratings up - but also my eyebrows as the long scene between the two (in which he berated her for not telling him his son was in prison for murder) left me rigid with tension. I found myself desperately asking: when is Deirdre going to cry real tears? She never did and as we went to an ad break, I decided to draw up the 10 questions I always seem to ask whenever I watch a soap. The first is obviously:
1 WHY CAN'T SOAP STARS CRY REAL TEARS?
Berated by an angry Ken for keeping Peter's arrest a secret, Deirdre's face screwed up and the cigarette--soaked voice dropped to an even raspier croak. She sobbed as if someone had stolen her collection of chainmail jumper belts. Ken shouted louder (Roache was magnificent - seemingly storing up all his acting skills during the six--month hiatus and unleashing them like a pensioner possessed).
Deirdre strained and croaked some more but still no tears emerged. Her mascara remained unsmudged, her blusher unstreaked. And I started laughing. Because it totally undermined the power of the scene. The actress Anne Kirkbride has played Deirdre in Coronation Street for long enough to have learned that she needs to cry quite often. But she can't.
Has no one on the Corrie team thought of dabbing her cheeks with glycerine or squirting some water in her eye?
Has no one on the Corrie team thought of dabbing her cheeks with glycerine or squirting some water in her eye?
2 WHY DO THEY HAVE TO WALK INTO PUBS AND SHOUT AT EACH OTHER?
I have never seen anyone verbally accosted by a neighbour or a friend in real life but it happens with exhausting regularity in soapland. You can bet your licence fee that if there is a secret to be kept or a wrong to be righted, someone will bellow it over the bar. If someone shouted at me in public I would never, ever speak to them again. Chances are that in the Queen Vic, The Rovers Return or the Woolpack, they'll be bonding over a cuppa before you can say "last orders."
3 WHY DO THEY THROW FOOD AWAY OR LEAVE IT UNTOUCHED AFTER A MINOR CONTRETEMPS?
One character comes in just as the pie and chips are being slapped on the table and says something innocuous such as "Why didn't you answer your phone when I rang you?" and before you know it, yet another perfectly good dinner has been scraped into the bin.
Throwing away good food is particularly unfathomable because every five minutes they're complaining that they are desperately hard up. Has nobody heard of clingfilm?
4 WHY ARE THE WOMEN STRONG AND THE MEN USELESS?
It's extremely rare to find a male character in the soaps who is strong, honest and attractive. Most of the women, on the other hand, could run the country. The men are as emotionally and financially responsible as primary school kids.
10 things that always happen in soaps but never in real lifeAnother quiet night in Emmerdale's Woolpack... [ITV]
5 WHY DO THEY ALWAYS HAVE MONEY FOR A DRINK AND A HOTPOT?
"We can't afford it", "money is tight", "we've got the bailiffs in", is a constant soap theme yet they always have enough for a pint or two. And why, when most of them live in the same street and presumably have a kettle, a jar of instant and a loaf in the kitchen, do they inevitably congregate over a huge breakfast in the café? Follow that with a meal at the bistro and chances are they've shelled out at least £100 - because they certainly don't stint on the drinks. So don't tell me you're hard up, soapies, when you eat out more often than Joan Collins.
6 WHY DO THEY NEVER LISTEN WHEN SOMEONE SAYS 'I'VE GOT SOMETHING TO TELL YOU'?
If someone said that to me I'd drop everything and panic. "What?! What is it?!" Nine times out of 10, if a soap character says: "Sit down, there's something you need to know..." the response is: "It'll have to wait, I'm going to Freshcos/Oh look there's Gail. I need a word/ Is that the time? Gotta go back to work." Those of us watching know it's important so why don't they?
7 WHY DO THEY NEVER WATCH TV?
Or go to the lavatory?
8 WHY ARE THEY SATISFIED WHEN A PARTNER SAYS HE/SHE IS GOING 'OUT FOR A BIT'?
If my husband said in the middle of the evening that he had to go out for a bit, I'd jolly well want to know where and with whom. In soapland there's no explanation, it always seems to be accepted by their other half. But often it does mean "for a bit". On the side. It might suit the storyline for a partner not to be suspicious but it doesn't ring true.
10 things that always happen in soaps but never in real lifeDenise leaves Albert Square with all her possessions neatly packed into one suitcase [BBC]
9 WHEN A CHARACTER LEAVES, WHY DO THEY HAVE ONLY ONE SUITCASE?
Surely it takes longer than one commercial break to put your affairs in order, sort out your wardrobe and dispose of your knick--knacks? But no. The decision to leave often comes a couple of sentences before we see them heading down the street with a poignant backward glance or gloomily gazing from the back of a taxi. Most people need at least a month to pack up and hire a van, arrange with the Post Office to forward the mail - even if they have lived there only a short time. How come they always walk out with one suitcase which seems no heavier than a gym bag and then never come back for the rest?
10 WHY CAN'T THE CHARACTERS SEE WHAT THE REST OF US CAN SEE?
"He's lying! He's never going to do what he says!" we shout at the TV. But still some pretty strong and bright soap women will say: "OK, if you need to go to Birmingham to work and won't be able to phone because you don't know the address of where you're staying or when you'll be back, that's fine."
Well it's not fine, lady, and you're deranged if you think he is telling the truth.
Yet still we watch and more infuriating questions spring to mind each time we tune in. And here's another one - why don't they ever discuss soaps like the rest of us?

Friday, 18 July 2014

Je ni sawa kwa Bangi kuhalalishwa kama chakula nchini?


Watu wa Makete hutumia mbegu za Marijuana kukaangia chakula tangu zamani
Huku harakati za kutaka matumizi ya Bangi kuhalalishwa zikishika kasi katika sehemu mbali mbali duniani, Tanzania haijaachwa nyuma.
Wanakijiji katika wilaya ya Makete , mkoa wa Njombe Kusini Magharibi mwa Tanzania wanataka serikali iweke sheria ambayo itaweza kuhalalisha matumizi ya mmea huo.
Wanakijiji hao zamani walikuwa wakitumia mbegu za mmea huo kukaanga na chakula lakini siku hizi wanalazimika kuzitumia kwa usiri mkubwa wakihofia kukamatwa na polisi.
Mwenyeketi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Daniel Okoka amesema matumizi ya Bangi katika wilaya hiyo hayajaanza leo, tangu zamani watu kitamaduni walikuwa wakitumia Mbegu za Bangi kukaanga na chakula.
Na kama mmea huo ungekuwa na tahri kubwa kiafya, basi watu wengi wilayani humo wangekuwa vichaa.
Majimbo mengi nchini Marekani yemahalalisha utumiaji wa Marijuana kwa sababu za kujistarehesha
Miti ya mimea hiyo pia ilikuwa ikitumiwa kutengeza kamba ambazo anasema zilikuwa za nguvu sana.
Lakini kwa sababu ya sheria kali, matumizi ya Bangi au Marijuana yanafanywa kichinichini katika wilaya hiyo.

Wednesday, 16 July 2014

BRICS kuwa mkombozi wa AFRIKA?

Viongozi wa nchi za BRICS wakati wa uzinduzi wa Benki Mpya ya Maendeleo huko Fortaleza, Brazil . (15.07.2014)
Viongozi wa nchi za BRICS wakiwa Fortaleza, Brazil . (15.07.2014)
Viongozi wa mataifa yanayoinukia kiuchumi BRICS yameanzisha benki ya maendeleo yenye thamani ya dola bilioni 100 katika hatua ya kuubadili mfumo wa fedha wa kimataifa unaohodhiwa na mataifa ya magharibi.

Benki hiyo inayokusudia kugharamia miradi ya miundo mbinu katika nchi zinazoendelea makao yake makuu yatakuwa mjini Shanghai China na India itasimamia shughuli zake kwa miaka mitano ya kwanza ikifuatiwa na Brazil na baadae Urusi.
Viongozi wa mataifa ya BRICS pia wameunda mfuko wa akiba utakaokuwa na uwezo wa dola bilioni 100 kukabiliana na shinikizo za kifedha.Benki hiyo ilokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu itaitwa Benki ya Mpya ya Maendeleo.
Hayo ni mafanikio ya kwanza makubwa ya nchi zinazounda BRICS za Brazil,Urusi,India,China na Afrika Kusini tokea zilipokutana mwaka 2009 kushinikiza kuwa na sauti kubwa katika mfumo wa fedha duniani ulioanzishwa na mataifa ya magharibi baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na kujikita katika Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia.
Ushawishi wa BRICS
Mataifa hayo yanayoinukia kiuchumi yalilazimika kuratibu hatua hiyo ya pamoja kufuatia kuhamishwa kwa mtaji kutoka katika nchi zinazoinukia kiuchumi mwaka jana kulikosababishwa na hatua za kuchochea uchumi za Marekani.
Benki hiyo mpya inaonyesha kuongezeka kwa ushawishi wa mataifa hayo yanayounda BRICS ambayo kwa jumla yana nusu ya idadi ya watu duniani na pato la kiuchumi duniani la takriban asilimia 20.

Benki hiyo itaanza na mtaji wa kuandikisha wa dola bilioni 50 ukigawiwa sawa sawa kati ya mataifa mtano waasisi wa BRICS na dola bilioni 10 taslimu zitakazotolewa awali katika kipindi cha miaka saba pamoja na dhamana za dola bilioni 40. Benki hiyo itaanza kutowa mikopo hapo mwaka 2016 na kupokea wanachama wa nchi nyengine lakini mgao wa mtaji wa mataifa ya BRICS katika benki hiyo haupaswi kushuka na kuwa chini ya asilimia 55.
Mbadala wa ushawishi wa Marekani

Taasisi hiyo inabidi iridhiwe na mabunge wa nchi za BRICS.
Rais Dilma Rousseff wa Brazil ameweka wazi uwezekano wa kutumia fedha za benki hiyo kuzisaidia nchi nyengine ambazo sio wanachama wa BRICS.
Leo viongozi wa mataifa hayo ya BRICS watakuwa na mkutano wa kilele na marais wenzao wa Amerika Kusini kutafuta njia mbadala za kukabiliana na ushawishi wa Marekani katika eneo hilo la Amerika Kusini.
Mataifa yatakayohudhuria mkutano huo ni pamoja na Argentina,Chile,Colombia, Ecuador na Venezueala.

Tuesday, 15 July 2014

Baada ya kusherekea miaka 50 ya umoja wa kisiasa na uchumi.Je Afrika tuko wapi katika maendeleo kutokana na neema tulizonazo?





Afrika inasherehekea miaka 50 ya umoja wa kisiasa na uchumi unaonawiri, ambapo bara hilo kwa muda mrefu sasa linaangaliwa kama eneo la neema kubwa, licha ya ukuaji huo wa kiuchumi kuwa na walakini.
Bara la Afrika linasherehekea hivi sasa miaka 50 ya Umoja wa Afrika kwa ufanisi tangu wa kisiasa mpaka wa kiuchumi. Bara hilo linajitokeza kama eneo lenye fursa kubwa ya kuwavutia wawekezaji. Baada ya "Chui wa Asia" sasa Simba wa Afrika wananguruma.
Takwimu zinadhihirisha uchumi utakuwa mwaka huu kwa 7% au zaidi katika robo ya mataifa yote ya eneo la kusini mwa jangwa la Sahara. Wakati huo huo, mengi ya mataifa hayo yamo katika lile kundi la mataifa ambayo uchumi wake unakuwa haraka kupita kiasi.
Waafrika wawili kati ya watano wana simu ya mkononi au Smartphone. Nguvu za ununuzi zinazidi kukuwa barani Afrika na masoko yanaongezeka, huku matajiri wakizidi kuongezeka barani humo. Huu ni ufanisi wa kusisimua ambao watu wanapenda kuuzungumzia – naiwe wanasiasa, wanauchumi na pia vyombo vya habari.
“Afrika inajikwamua“, anasema mwandishi habari wa masuala ya kiuchumi Anver Versi. Mkenya huyo anaemiliki jarida la kiuchumi la African Business Magazine linalochapishwa mjini London anasema: "Kuna sababu nzuri za kuhoji kwamba Afrika itageuka kuwa soko muhimu la ukuaji wa kiuchumi katika miaka 50 inayokuja .Kwa sababu Afrika ina mali ghafi na nguvu kazi. Mtu anaweza kusema Afrika ni mahala pa kuvutia kabisa kuwekeza hivi sasa - Wachina wameitambua hali hiyo tangu miaka 10 au 15 iliyopita. Na sasa wajasiriamali wa Kijerumani na wazungu kwa jumla wanabidi wazindukane na kuitambua fursa hiyo."
Matumaini yana walakini

Katuni ya maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika.
Kwa mujbu wa makadirio ya Benki Kuu ya Dunia, uchumi katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara utakuwa kwa kadiri ya 5% katika kipindi cha mwaka 2013 na 2015. Uchumi wa dunia katika kipindi hicho hicho utakuwa kwa kadiri ya 3% tu.
“Viwango hivyo ni vya juu vya ukuaji wa kiuchumi, lakini hiyo bado si sababu ya kushangiria,“ anasema Robert Kappel. Mtaalam huyo wa Kijerumani anayeshughulikia masuala ya utafiti wa masuala ya Afrika katika taasisi ya GIGA mjini Hamburg, amechunguza makadirio ya ukuaji wa kiuchumi katika mataifa 42 ya kusini mwa jangwa la Sahara. Mengi ya mataifa hayo hayatofua dafu kwa mlinganisho wa kimataifa.
Robert Kappel anasema: "Ukuaji unatokana zaidi na ile hali kwamba mahitaji ya mali ghafi na bidhaa za mashambani yameongezeka sana katika kipindi cha miaka iliyopita na kwa namna hiyo bei nazo zimepanda. Kwa hivyo, inamaanisha biashara ya nje inachangia sana katika ukuaji wa kiuchumi barani Afrika na huo ni udhaifu mkubwa."
Taasisi kuu za fedha duniani, Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki Kuu ya Dunia, zote zinaonya juu ya bara la Afrika inategemea sana biashara na nchi za nje. Naye Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, aliyataka mataifa ya viwanda katika Kongamano la Kiuchumi la Kimataifa hivi karibuni mjini Cape Town nchini Afrika ya Kusini yawekwe sheria kali katika biashara ya mali ghafi pamoja na Afrika. “Rushwa na kukwepa kulipa kodi za mapato,“ anasema Kofi Annan, “ndio chanzo cha kudhoofika neema barani Afrika.“
Nini cha kufanya kuimarisha uchumi?
Mchoro wa maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika.
Shughuli za viwanda zinazorota barani Afrika na kilimo hakitoshi hata kukidhi mahitaji ya wakaazi wa bara hilo. Hata katika soko la ajira hakuna ishara ya kuongezeka nafasi za kazi. Hata katika nchi inayonyanyukia kiuchumi ya Afrika ya Kusini, zaidi ya 25% ya wakaazi wake hawana kazi na wanaoathirika zaidi ni vijana wanaoishi mashambani.
Kwa hivyo, nini cha kufanya ili ukuaji wa kiuchumi barani Afrika utuwame katika msingi imara? Mwandishi habari wa masuala ya kiuchumi, Anver Versi, anahisi panahitajika vitega uchumi zaidi katika miundo mbinu. Naye Robert Kappel wa Taasisi ya Uchunguzi wa Masuala ya Afrika anahisi mageuzi ya kiuchumi pia yanahitajika pamoja na sheria bora za uwekezaji ili kuwavutia wateja tangu wa ndani mpaka wa kimataifa.