Showing posts with label Entertainment. Show all posts
Showing posts with label Entertainment. Show all posts

Friday, 8 August 2014

Wema sepetu afunguka kuhusu kuzaa..........!!

Wema Leo Ameamua Kuwafungukia Wale wanaopenda kumforce azae, Wema aliweka Picha ya Kim Kardashian akiwa amembeba Mtoto wake na Kuandika Mbona Huyo Kazaa akiwa Miaka ya 30 sasa kwanini watu wanamforce wakati yeye bado yupo 20′s Jisomee Mwenyewe hapo chini:
wema

Jack Wolper adaiwa kutibua Uchumba wa Nay Wa Mitego na Siwema

Mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefungukia madai ya kutoka na msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper na kudai kuwa wao ni washikaji tu ila ukaribu wao umesababisha mtifuano kati yake na mchumba wake, Siwema.
ney kimwana Akizungumza na mwandishi Nay alisema, watu wamekuwa wakieneza kuwa yeye na Wolper wanatoka kiasi cha kumkosesha amani Siwema na kufikia wakati f’lani wakatibuana.
 
 Mahojiano kati ya mwandishi wetu na Nay yalikuwa hivi: 
 
Mwandishi: Kuna madai kuwa wewe unatoka na Wolper, hii ikoje?
Nay: Wolper ni mshikaji wangu, kama watu wanavyojua kwamba yule ana mambo ya kisela f’lani na hicho ndicho kinanifanya nimpende. 
 
Ila najua kitu kilichowafanya watu wahisi kuna kitu kati yangu na yeye ni baada ya kuposti picha yangu kwenye ukurasa wake wa Insta na hapo ndipo likaibuka tatizo. Na hilo lilileta ugomvi kwenye uhusiano wangu lakini ukweli ni kwamba kama mahusiano yapo ni ya kawaida tu.
Jackline  Wolper
Jackline Wolper
Mwandishi: Sasa wewe na Wolper mkikutana huwa mnazungumzia nini?
Nay: Mambo ya kazi tu, si unajua nina mpango wa kucheza muvi baadaye

Mwandishi: Mbona sasa inadaiwa mnatoka kwa siri?
Nay: Hayo maneno ya watu tu japokuwa ni mwanamke mzuri, anamvutia mwanaume yoyote rijali
 
Mwandishi: Ikitokea ameingia mzimamzima kwako itakuwaje?
Nay: Ikitokea ameamua kuingia mzimamzima, nitaangalia mapokeo yake (Kicheko sanaaa)
 
Mwandishi  alifanya jitihada za kumsaka Wolper kupitia simu yake ya mkononi lakini hakuweza kupatikana.

Thursday, 7 August 2014

Anti Ezekiel afunguka kuhusu kutoka na dansa wa Diamond


Mwanzoni mwa wiki hii miongoni mwa stori ambazo zilitoka na kuenea kwenye magazeti kadhaa ni pamoja na inayomhusu Anti Ezekiel kusemekana kuwa anatoka na dansa wa Diamond Platnumz.
Taarifa ya awali ilidai kuwa mpenzi huyo wa dansa wa Diamond alienda kufanya vurugu nyumbani kwa Anti Ezekiel,Anti Ezekiel kapatikana na kaongelea mahusiano yake na Moses Iyobo ambaye ndiye dansa wa Diamond Platnumz.

Ali Kiba ampa ushauri Tunda Man baada ya kuugua ghafla

Mwimbaji wa Tip Top Connection, TundaMan aliwashangaza wengi baada ya kueleza kuwa alipokea simu yenye namba nyingi asizozielewa na ghafla akapata mshtuko na kuishiwa nguvu, hali iliyomsababisha akimbizwe hospitali ambapo alipewa matibabu.
 
Licha ya kuwa wataalam na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) walieleza wazi kuwa kitaalam simu haiwezi kabisa kuwa chanzo cha tatizo hilo, TundaMan alisisitiza kuwa yeye ndiye aliyepata tatizo na anajua kilichotokea.
 
“Wao wanasema haiwezekani kwa sababu hilo tatizo halikuwakuta…lakini kwa kuwa mimi ndiye nimekuwa affected kwa siku mbili tatu, mimi naamini kuwa tukio hilo lipo na limekuja baada ya kupokea ile simu. Wao wanaongea kitaalam siwezi kubishana nao, lakini mimi limenikuta na nimeona.” Amesema  Tundaman
 
Kutokana na sintofahamu hiyo, Tundaman ameeleza kuwa msanii mwenzake, Ali Kiba alimshauri kwenda katika nyumba ya ibada ili apate dua maalum.
 
“Yeah inawezekana (ni ushirikina) kwa sababu vitu kama hivyo huwa vinatokea sana na ndio maana ndugu yangu Ali Kiba amenishauri nikapate dua.” Amesema Tunda Man.
 
Ameeleza kuwa tayari amechukua uamuzi huo ingawa hali yake pia inaendelea kuimarika baada ya kupata matibabu.

Wiz Kid amjibu Davido kupitia twitter

Jana Davido alizungumzia kitu gani kilimkasirisha hadi bifu na Wiz Kid kutokea, Wiz ameingia twitter na kumjibu bila kumtaja jina kama kawaida yao. Tweet hiyo inadhihirisha kwamba Wiz Kid hakupenda jinsi Davido alivyozungumza kuhusu hilo beef.kid

Wednesday, 6 August 2014

Aunt Ezekiel anusurika kupigwa nyumbani kwa Wema

Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson anadaiwa kukinukisha nyumbani kwa Wema Isaac Sepetu baada ya kunusurika kufumaniwa na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo a.k.a Moze Iyobo ambaye ni densa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Habari za kuaminika  zinadai kwamba tukio hilo lilitokea hivi karibuni nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, Dar ambapo Aunt alisababisha tafrani iliyosababishwa na mke wa mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Mwengi Ally.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu waliokuwa wakizungumza kwa kupokezana, Mwengi alidai kwamba Aunt amekuwa akitembea na mumewe huyo hivyo timbwili lilianzia nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala A jijini Dar.
Ilidaiwa kwamba, huku Aunt akiwa hajui hili wala lile, ghafla waliibuka wasichana saba na kumuanzishia mwigizaji huyo.Mashuhuda hao walidadavua kwamba katika kujinusuru na kipigo ambacho alihisi akiwa peke yake, angeumizwa Aunt alikimbilia  nyumbani kwa shoga yake, Wema.
Ilidaiwa kwamba wasichana hao hawakuishia hapo kwani walimkimbiza Aunt hadi wakamuona akiingia kwa Wema ambapo walipofika getini walikutana na meneja wa msanii wa Bongo Fleva, aitwaye Mirrow, Petit Man ambaye walimuomba amtoe Aunt ili wamshikishe adabu ajifunze kukaa mbali na waume za watu.
Ilisemekana kwamba katika tafrani hiyo getini, Wema alitoka na msichana wake aitwaye Careen lakini Aunt hakutoka ambapo waliwaambia wasichana hao kuwa Aunt hawezi kutoka na isitoshe wa kulaumiwa ni Moze Iyobo kwani yeye ndiye anayedaiwa kumtongoza Aunt na kuanza kuchati naye hadi mkewe akanasa meseji zao za mapenzi.
Baada ya kujazwa data hizo, Mwandishi alimtafuta Mwengi ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na ishu hiyo ambapo alikiri kwenda kwa Aunt na Wema lakini hakufanikiwa kumpata Aunt kwani kama angemkamata, maafa yangetokea.Mwengi alisema kuwa siku ya tukio aliitwa na Aunt maeneo ya Mlimani City, Dar na akamwambia aende na mtoto akamfanyie shopping.



Alisema baada ya kuambiwa hivyo hakuwa na hiyana kwani alijua kuwa ni kama mama yake mkubwa na shoga wa mpenzi wa baba yake mkubwa ambaye ni Diamond, kumbe nyuma ya pazia kulikuwa kuna kitu kingine kimejificha.“Niliporudi nyumbani, mume wangu aliniambia nimpige picha kwa kutumia simu yake, nilipoifungua ndipo ikaingia meseji kutoka kwa Aunt.
“Nilipoisoma ile meseji nikagundua kuwa walianza kuchati muda mrefu kuhusu mapenzi yao, ndipo nikakusanya jeshi langu na kumfuata nyumbani kwake nikamshikishe adabu, amshukuru Wema kumficha maana sipati picha kwa jambo ambalo lingetokea. Ingekuwa mwisho wake wa kupora waume za watu,” alisema Mwengi.
Alipotafutwa Aunt na kuulizwa juu ya sakata hilo, alijibu kwa kifupi: “Sina muda mchafu wa kuongea halafu nimelala, kwa sasa niache nipumzike.”

Rose Mhando anatamani kuwa na Gwajima.......!

Nyota wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando amesema anatamani sana kuhamia kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima kutokana na mahubiri yake mazuri. 
“Natamani nihamie katika kanisa la Mchungaji Gwajima lakini mimi huwa napenda kumuita Askofu kwa sababu ya upako alionao, naomba ikiwezekana na mimi nihamie hapa,” alisema Rose.
Mwanamuziki nguli wa nyimbo za injili, Bongo Rose Muhando.
Katika siku ambayo kulikuwa na sala ya shukurani kanisani kwa Gwajima Jumapili iliyopita Kawe jijini Dar es Salaam,  mchungaji huyo alimwambia Rose aliyealikwa kuimba, kwamba yupo tayari kumjengea kanisa Dodoma anakoishi na yeye mwenyewe alisimamie.

Monday, 4 August 2014

EXCLUSIVE: Chris Brown akana kutemwa na Karrueche .......!!!!!!!!!!!!




Kutokana na tetesi kwamba Chris Brown katemwa na aliyekuwa mpenzi wake Karrueche, madai hayo ameyakanusha na kusema kuwa yeye ndiye aliye mtema kimwana huyo.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ambavyo vipo karibu na wapenzi hao zinasema kuwa  Chris alishtushwa na habari zilikuwa kuwa zimeenea kwamba yeye kuachwa na Karrueche badala yeye kumuacha.

Taarifa hizo zilipo takiwa kutaja Sababu zinazodaiwa kuachwa kwa karrueche zinasema kuwa Chris alipogundua Karrueche alikuwa akichati na mwanaume mwingine na kutumiana picha wakati wakiwa pamoja mara.

Taarifa hiyo ilidai kuwa Brown alipatwa na hasira baada ya mwana dada huyo kufanya mahojiano katika maonyesho ya mavazi yake na kuzungumzia juu ya uhusiano wao
Ikumbukwe  Karrueche alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari huko Marekani ivi karibuni akisema kwamba licha ya Chris kuendelea kuwa karibu na Rihhana lakini kinacho muhudhi zaidi ni kwamba bado anavitendo vya kitoto na kuendekeza sana bata na wanawake kuliko shughuli zake za muziki kitu ambacho amekichoka.


Ali Kiba: Lulu Michael anafaa kuwa MKE

Kwa mara ya kwanza, staa anayeitikisa nchi kwa sasa na wimbo wake wa Mwana, Ali Kiba amefunguka kuwa mwigizaji kiwango Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ anafaa kuwa mke (wife material) huku akiweka wazi sifa kibao alizonazo. 
Kiba ambaye hivi karibuni ameibua mijadala mingi katika mitandao ya kijamii, usafiri wa umma na kwenye baa juu ya ujio wake mpya akisemekana kurudia kiti chake ambacho alikikalia Mbongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’ kwa muda, mwaka 2010 aliwahi kuripotiwa kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na Lulu ambaye wakati huo alikuwa na umri chini ya miaka 18!
 

LULU ANAFAA KUWA MKE

Akizungumza na Globa TV Online mwishoni mwa wiki iliyopita, Kiba  alisema Lulu anafaa kuwa mke kwa vile ni mchapakazi sifa ambayo mke mwema anapaswa kuwa nayo.
 

AMMWAGIA SIFA

Kiba alisema Lulu anajua kuhangaika, anajua kupambana kusaka pato lake kihalali kupitia mauzo ya sinema zake anazozizalisha kitu ambacho kinawashinda mabinti wengi na kuangukia katika biashara ya kuuza miili (ukahaba).
 
Licha ya kummwagia sifa hizo, kipindi hicho alichokuwa akitajwa kuwa naye, Lulu alikuwa na matukio ambayo hayakuwa na maadili lakini Kiba hayo hakuyatilia maanani. 
 
Mwandishi: Unafikiri Lulu ni ‘wife material’ (mke mwema) ambaye unaweza kumweka ndani akalea watoto na kuijenga familia bora?
Kiba: Yeah! Anafaa kuwa mke, ni binti anayejituma, mchapakazi, mtafutaji. Kwangu mimi mtu wa namna hiyo ndiyo anafaa kuwa mke.
 
Mwandishi: So, unataka kutuambia kwamba unaweza kumuoa?
Kiba: Sijasema hivyo mimi, nimesema anafaa kuwa mke.
 

ACHOMOA KUBANWA KISHERIA

Licha ya kuchomoa ishu hiyo ya uhusiano, waandishi wetu walimbana zaidi staa huyo afafanue kwa nini alitajwa yeye na si msanii mwingine huku ikidaiwa kuwa, Lulu hakuwa ametimiza miaka 18 hivyo kubanwa kisheria (ya watoto na kujamiiana).
 
“Sijatembea naye ndiyo maana unaona hata sheria haijanihukumu, endapo ningekuwa nimetembea naye, basi sheria ingeweza kunitia hatiani na ningefungwa jela,” alifafanua Kiba.
 

AWASHANGAA WANAOMSHANGAA

Kiba aliongeza kuwa, anashangaa sana kuona watu wanamsema vibaya yeye kupendwa na Lulu.
 
“Lulu ni msanii mwenzangu, anapenda kazi zangu na mimi napenda za kwake. Ni rafiki wa kawaida, hakuna kitu kingine cha ziada. Nawashangaa wanaozusha ya kuzusha, hivi kwani kuna tatizo Lulu akinipenda? Sidhani kama ni kosa, ana haki ya kunipenda kutokana na muziki wangu.
 
“Unajua muziki mzuri huwa unapenya automatically, huwezi kuzuia hisia za muziki, mtu unaweza ukawa humpendi msanii f’lani lakini ukapenda muziki wake, unajikuta tu unampenda, unaanza kuimba nyimbo zake,” alisema Kiba.
 

KUMBUKUMBU MBICHI

Juzikati wakati Kiba anatambulisha nyimbo zake mbili kwa mpigo (Mwana na Kimasomaso), Lulu, kupitia mtandao wa Instagram alitupia maneno ya kummwagia sifa staa huyo, liliibuka kundi ambalo linatajwa kuwa ni wafuasi wa mwigizaji Wema Sepetu ‘Team Wema’ na kuanza kumshambulia kwa maneno machafu.
 

KIBA AFUNGUKA

Akizungumzia ishu hiyo, Kiba alisema waliofanya hivyo hawakumtendea haki Lulu kwani ana haki ya kueleza hisia zake pale anapoguswa na muziki mzuri.
“Hawajatenda haki kwa sababu Lulu ni binadamu kama walivyo wengine, ana haki ya kupenda kitu kizuri,” alisema Kiba.

KUHUSU KIFO CHA KANUMBA

Kiba akizungumzia juu ya kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa nyota wa sinema Bongo, marehemu Steven Kanumba ambapo alidaiwa kunaswa kwa meseji za mapenzi alizozituma kwa Lulu ndiyo zilizosababisha mtifuano ambao ulisababisha kifo cha Kanumba, alikana madai hayo.
 
“Si kweli, sikuwa nimewasiliana na Lulu siku hiyo kabla ya tukio. Nakumbuka nilikuwa safarini, baada ya tukio nilimpigia Lulu kutaka kujua ukweli wa taarifa za kifo kwa sababu marehemu alikuwa mtu wangu  wa karibu kama alivyo Lulu,” alisema Kiba.
 

AMGUSIA WOLPER

Kwenye mahojiano hayo, mkali huyo alizungumzia ishu ya mwigizaji, Jacqueline Wolper kukiri kwamba Kiba ndiye mwanaume aliyemtoa usichana wake kwenye simulizi iliyochapishwa katika Gazeti la Championi hivi karibuni.
 
“Mh! Aliwahi kukiri? Daah! Sijui bwana… Wolper ni mtu wangu wa karibu kama alivyo Lulu,” alisema kwa mkato Kiba.

Saturday, 2 August 2014

Shilole na NUH wanaswa Live Chumbani Akingonoka

Picha za staa wa sinema na Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole Kiuno’ zinazomuonesha live akiwa chumbani tena kitandani kimahaba na mwandani wake, Nuh Mziwanda zimevuja…. Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa Shilole, picha hizo walijipiga wenyewe wakiwa kitandani nyumbani kwa mwanadada huyo, Kinondoni jijini Dar.
Chanzo hicho kilidai kwamba picha hizo walijipiga baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani kabla ya hapo wasingefanya hivyo.
Katika picha hizo zinazowaonesha wawili hao wakiwa katika mahaba niue, Shilole anaonekana akiwa amemlalia Mziwanda ambaye naye amejiachia vya kutosha.

Habari za ndani zinadai kwamba mmoja wa watu wa karibu alishika simu ya Shilole kisha akajifowadia picha hizo ndiyo chanzo cha kumfikia mtu wetu huyo.

Baada ya kuzidaka picha hizo, mwandishi alimtafuta Shilole ambaye kwa sasa anakimbiza na ngoma yake mpya ya Namchukua ambapo alipopatikana kwa njia ya simu alisomewa mashitaka yake ndipo akafunguka namna alivyochezewa na mtu wa karibu yake.
“Kweli hizo picha ni zangu na Nuh (Mziwanda), tulijipiga kwa ajili ya kumbukumbu na tulikuwa na muda mrefu hatujiachia si unajua tena Mwezi Mtukufu?
 
“Unajua simu yangu haina password na nina watu wengi wa karibu so nahisi ndiyo wamezivujisha na nikimjua namtoa kabisa kwenye network yangu maana siku nyingine anaweza kunifanyia jambo kubwa baya.”

Davido atangaza Ngoma mpya aliyomshilisha mkali kutoka Maybach Music Group



Skelewu, Gobe, Ekuro,One of a kind,Aye ni baaadhi ya nyimbo ambazo zinamuweka Davido kwenye chati ya muziki na kumsaidia kushinda tuzo mbalimbali kama BET,MTV na nyingine nyingi.
Wiki ijayo mashabiki wa Davido wanatajia kupata kusikiliza nyimbo mpya kutoka kwa Davido akiwa pamoja na member wa MMG anayetambulika kwa Wale. Wimbo unaitwa Won Le Ba na taarifa hii imeripotiwa na Davido mwenyewe.

Friday, 1 August 2014

EXCLUSIVE:Karrueche Tran na Chris Brown kuachana




Vyanzo mbalimbali majuu vimeripoti yanayoendelea katika mahusiano ya Chris Brown na mwana dada Karrueche vikisema Karrueche alishtukia mbinu chafu ya  Chris hivi karibuni alipo "like"picha mbili za shabiki  kwenye Instagram ya Rihanna wakati wakiwa pamoja.


Hata hivyo Rihanna alikuwa ni sehemu ndogo ya matatizo yaliyojitokeza kwa Karrueche  na Chris.

Taarifa hiyo inasema kuwa kwa muda mrefu Karrueche alikuwa hana raha ...huku ikidaiwa kuwa kwa sababu Chris kuwa na vitndo vya kitoto mara kwa mara na kutumia muda mwingi kupati kuliko kufanya shughulizake za muziki
“Chris act immature,like child and he’s ruining his life by spending more than making music”alinukuliwa Karrueche.

Vyanzo hivyo vya habari vinasema kuwa vitendo vya chris vimekuwa vya kukatisha moyo.ikiwa wiki hii alikwenda St Tropez na kumchukua ratokanae huku mwenyewe akiwa hajui.

Pia vyanzo hivyo vinasema kuwa Maamuzi ya Karrueche si jambo la  wivu kwa kuwa aliamua kubadili namba ya simu yake ya zamani ili hasiweze kuwasiliana na Chris na inaweza kuchukuwa muda mambo kuwa sawa.