Monday, 28 July 2014

Bado mzimu wa Ghadaf waendelea kuitesa Libya


Kiasi ya watu 150 wameuawa katika ghasia ambazo zimezuka upya katika miji ya Benghazi na Tripoli katika kipindi cha wiki mbili zilizopita kufuatia makabiliano makali kati ya wanajeshi na makundi hasimu ya wanamgambo.
Wizara ya afya ya Libya imesema tangu makabiliano hayo kuzuka wiki mbili zilizopita, kiasi ya watu 94 wameuawa katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli na zaidi ya wengine 400 wamejeruhiwa wakati wa mapambano kati ya wanajeshi na wanamgambo wanaong'angania kuudhibiti mji huo.
Kiasi ya wengine 55,wengi wao raia wameuawa katika mji wa Benghazi mwishoni mwa juma katika makabaliano mengine kati ya jeshi na makundi ya wanamgambo wa kiislamu.
Maroketi yalenga mapipa ya mafuta
Shirika la taifa la mafuta limesema maroketi yaliyokuwa yakirushwa, yalilenga matangi ya kuhifadhia mafuta karibu na uwanja wa ndege wa Tripoli hapo jana na kusababisha moto mkubwa ambao wazima moto wameshindwa kuuzima. Matangi hayo yalikuwa yanahifadhi kiasi cha lita milioni sita za petroli na yako karibu na mengine yanayohifadhi gesi na diesel.
Abiria wakisubiri kusafiri katika uwanja wa ndege wa Miitiga
Wizara ya mafuta na nishati imewaonya raia wanaoishi karibu na maeneo ya matangi hayo kuondoka mara moja kuepusha majanga ya kibinadamu na kimazingira kufuatia kuzuka kwa moto huo mkubwa.
Mapigano hayo ya wiki mbili ndiyo mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo tangu kung'olewa na baadaye kuuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa tafa hilo Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Marekani,Umoja wa Mataifa na Uturuki zimewaondoa wafanyakazi wa balozi zao kutoka taifa hilo la kaskazini mwa Afrika. Marekani iliwahamishia wafanyakazi hao katika nchi jirani ya Tunisia siku ya Jumamosi chini ya ulinzi mkali baada ya mapigano kupamba moto karibu na ubalozi wake mjini Tripoli.
Msafara wa magari yaliyokuwa yamewabeba maafisa wa Uingereza ulishambuliwa jana katika jaribio la utekaji nyara nje ya mji wa Tripoli ulipokuwa ukielekea Tunisia na ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa katika kisa hicho, magari yaliharibiwa.
Wajumbe maalumu wa jumuiya ya nchi za kiarabu kuhusu Libya,Marekani na umoja wa Ulaya wameelezea wasiwasi wao kuhusu hali inavyozidi kuzorota nchini Libya na kusema hali hiyo imefikia hatua ngumu na kutaka mapigano kusitishwa mara moja.
Nchi za magharibi zawataka raia wake kuondoka
Ujerumani, Uingereza ,Ufaransa, Uholanzi, Ubelgiji, Misri na Uturuki nimiongoni mwa nchi nyingine ambazo zimewataka raia wao walioko Libya kuondoka nchini humo mara moja kwa sababu ya kudorora kwa hali ya usalama.
d Wapiganaji wa kundi la wanamgambo la Misrata
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amesema raia wa Ujerumani walioko Libya wako katika hatari kubwa ya kutekwa nyara na kuuawa kwa sababu sio rahisi kutabiri hali nchini humo itachukua mkondo gani.
Bunge jipya la Libya lililochaguliwa mwezi Juni mwaka huu linatarajiwa na nchi za magharibi kuwa litaweza kumaliza mzozo huo kwa kufikiana makubaliano ya kisiasa wakati wabunge watakapokutana kwa kikao cha kwanza mwezi ujao.
Miaka mitatu baada ya kung'olewa kwa Gaddafi,ndoto ya Libya kuifikia demokrasia imezongwa na malumbano ya wenyewe kwa wenyewe ya kisiasa na mapigano ya mara kwa mara kati ya makundi hasimu ya waasi waliosaidia kumuondoa Gadafi madarakani ambayo yanataka kuidhibiti miji mikuu na viwanda vya mafuta.

KOREA KUSINI:Wanafunzi wafichua mkasa mzima uliosababisha meri kuzama




Wanafunzi walionusurika katika mkasa wa feri iliyozama nchini Korea Kusini mwezi Aprili wamesema kuwa waliagizwa kusalia katika vyumba vyao wakati meli hiyo ilipozama .
Walikuwa wanatoa ushahidi katika kesi inayomkabili nahodha na wafanyikazi wa meli hiyo wanaokabiliwa na mashtaka ya uzembe na mauaji kufuatia kufa maji kwa takriban watu 300 katika mkasa huo.
Mwanafunzi mmoja amesema kwamba yeye na wenzake walifuata maagizo hayo hadi pale mlango wa chumba chao ulipokuwa juu ya vichwa vyao huku maji yakiingia ndani ya feri hiyo kupitia madirishani.
Mwengine alitaka kujua ni kwa nini waokoaji hawakuingia ndani ya chombo hicho ili kuwasaidia kutoka.
Wanafunzi walikaribia kwenye milango ya kutoka ambapo walisaidiwa kutoka na wanafunzi wenzao.
Feri hii ilizama tarehe kumi na sita mwezi wa Aprili kwenye kisiwa cha Jeju ambapo watu mia tatu na wanne waliaga dunia.
Wanafunzi hao walikuwa wakitoa ushahidi katika kesi wanohukumiwa wafanyikazi wa feri hiyo.
Tulikuwa tumengoja hadi wakati ambapo maji yalianza kuingia kwenye feri ,msimamizi wa darasa alituagiza kuvaa vazi maalum la kuokoa maisha.mwanahabari wa Reuters aliiga maneno ya mwanafunzi .
Wanafunzi wananza kutoa ushahidi Korea
''Kupitia mlango uliokuwa juu yetu tuliweza kuelea na hatimaye tukatoka.wanafunzi waliotoka mbele yetu walituvuta nje ya meli hiyo.''
Wengi wa Walioaga dunia kwenye meli hiyo ya Sowel walikuwa wanafunzi kutoka shule moja ya upili waliokuwa kwenye ziara ya shule.
Wafanyikazi wanashtumiwa kwa kosa la kutomakinika na kutelekeza majukumu yao .
Nahodha na maafisa watatu pia wanakabiliwa na kosa la mauaji kwa njia ya uzembe kwa makusudi.
Wachunguzi wanasema kwamba feri hiyo ilikuwa imeundwa kinyume na sheria ili iweze kubeba abiria na mizigo zaidi,hivyo basi ilikuwa imepitisha kiwango kinachostahili.
Hata hivyo waendeshaji mashtaka walisema kuwa tendo la nahodha na wafanyikazi kuwaagiza abiria kutulia humo ndani feri hiyo ilipokuwa ikizama kulisababisha vifo zaidi.
Jumatatu ilikuwa siku ya kwanza wanafunzi hao walikuwa wanatoa ushahidi .
Baadhi ya wanafunzi walionusurika
Mwanafunzi mwingine alieleza kutoweka kwake kwa kuruka kwenye bahari
Msichana mmoja alisema kuwa Kulikuwa na wanafunzi wengi katika ukanda wa meli ambao walizuiliwa kwenye feri hiyo.
Mkasa huu ulisababisha hasira nchini Korea Kusini ikiwemo ukosoaji mkali kwa wafanyikazi wa serikali na wanabiashara ambao wanasemekana kutowajibika katika kazi yao ama pia yawezekana ufisadi ulipelekea mkasa huo.
Mwaanzoni mwa mwezi huu,polisi walitambua maiti ya mwenye kampuni inayomilika meli hiyo Yoo Byungeun .
Mwanawe wa kiume Yoo Dae-Kyun alikamatwa ijumaa.

Kisanga kingine chatokea Nigeria baada ya Boka Haramu kutishia kutokea kwa milipuko ya magari.......!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari katika jimbo la Borno
Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari kwa siku tatu katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa taifa hilo ili kuzuia tishio la wanamgambo wa Boko Haram.
Msemaji wa jeshi amesema kuwa hatua hiyo itazuia utumiaji wa magari kutekeleza mashambulizi ya kujitolea mhanga wakati wa siku kuu ya Eid ul Fitr.
Wakati huohuo kumekuwa na ripoti ambapo mlipuaji wa kujitolea muhanga amewaua watu kadhaa katika mji wa kazkazini wa KANO.
dKundi la Boko Haram limetishia kulipua bomu la gari
Taarifa hiyo iliyotolewa hivi kalibuni ilisema kuwa Wanajeshi hao waliwashauri waislamu kuhudhuria swala za Eid karibu na viwanja vilivyopo karibu na makaazi yao kwa kuwa kundi hilo lilikuwa linapanga kutekeleza mashambulizi katika viwanja,masoko pamoja na maeneo mengine ya uma wakitumia magari.
Gavana wa Borno Kassim Shetima amesema kuwa anawaonea huruma maelfu ya watu waliolazimika kutumia mda wao mwingi kutembea hadi katika viwanja vya kufanyia salah,lakini akaongezea kuwa hatua hiyo inalenga kuwalinda .
Kundi la Boko haram linadaiwa kuiteka miji kadhaa kusini mwa Borno na kuweka bendera zake.
Jeshi la Nigeria hivi majuzi lilikiri kwamba baadhi ya wanajeshi wake walikuwa wanatoroka kutokana na uvamizi wa wanamgambo hao.

UPDATE: Picha Tatu za Bahati Bukuku akiwa Hospitalini baada ya kupata Ajali mbaya ya Gari


Nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Bahati Lusako Bukuku ameumia mgongo na maeneo kadhaa ya mwili (nusu kifo) kiasi cha kushindwa kukaa, kusimama wala kutembea kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea kwenye eneo la Ranchi ya Narco wilayani Kongwa, Dodoma saa tisa usiku wa kuamkia Jumamosi.Katika ajali hiyo ambayo Bahati alikuwa akienda Kahama, Shinyanga kwenye mkutano wa Injili, dereva wa gari alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT 7945, Edison Mwakabungu ‘Eddy’ (31) aliumia sana kwenye vidole vya miguu na hawezi kutembea.
Wengine waliokuwemo kwenye ajali hiyo ni wacheza shoo wa Bahati, Frank Muha (20) na mwenzake ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Alfajiri ya juzi, mwandishi wa habari hizi alimpigia simu Bahati na kuongea naye kuhusu ajali hiyo ambapo huku akisikika kama anayepata tabu kwa maumivu, alisema:

“Ni kweli tumepata ajali, nimeumia mgongoni, dereva ameumia mguu. Namshukuru Mungu. Sijui nini kilitokea, nilishtukia kuona gari kubwa mbele yetu likituvaa, mara nikashtukia tuko porini. Lakini kabla ya safari Dar tulifanya maombi makubwa, najua Mungu ametunusuru na kifo kibaya,” alisema Bahati.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa hii si mara ya kwanza kuripotiwa kwa ajali za magari mkoani Dodoma zikiwahusisha watu wa tasnia Injili Bongo.
Aprili, mwaka huu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama alipata ajali mbaya ya gari kwa kugongana na mwendesha bodaboda.Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Ipagala Mwisho, kilomita chache kabla ya kufika mjini Dodoma. Msama alikuwa kwenye gari lake aina ya Toyota Mark II GX 100.
Katika ajali hiyo, Msama na mwendesha bodaboda huyo waliumia sehemu mbalimbali za mwili na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu.

MAJANGA! Mke wa Kingwendu Abakwa…!

MKE  wa  Kingwendu  ambaye  ni  muigizaji  maarufu  wa  filamu  za  vichekesho  nchini  amefanyiwa  kitendo  kibaya  cha  ubakaji  na  mwanaume  aliyefahamika  kama  Upunguvuku  katika  pagala  moja  huko  Mbagala  Kingugi  kwa  Kisauti…..
 
Mke  wa  Kingwendu  anayejulikana  zaidi  kwa  jina  la  mama  Maua, alikutwa  na  masahibu  hayo  Alhamisi  iliyopita  baada  ya  kuvamiwa  na  Upunguvuku  anayedaiwa  kuwa  alikuwa  amelewa  na  kuingizwa  kwenye  jumba  ambalo halijasha  kujengwa  lililopo  maeneo  ya  Kwa  Dunga    ambapo  wapita  njia  waliwafuma  na  kuanzisha  mtiti…..
 
Shuhuda  wa  tukio  hilo  ambaye  hakutaka  jina  lake  liandikwe  amesema  kuwa, wakati  tukio  hilo  linatokea, Kingwendu  mwenyewe  alikuwa  safarini  na  hivyo  majirani  zake  ndio  waliomuokoa  mkewe……

 
Hata  hivyo  baadhi  ya  majirani  walioongea  na  mwandishi  wamedai  kuwa  wawili  hao ( Upunguvuku  na  mama  Maua)  ni  wapenzi  wa  siku  nyingi  na  wamekuwa  wakionekana  mara  kadhaa  wakienda  kunywa  pombe  za  kienyeji…..
 
“Huyu  Upunguvuku  ni  fundi  Mwashi, tunamfahamu  vizuri  kuwa  ni  hawara  wa  mama  Maua, mara  kadhaa  huwa  tunawaona  wakinywa  pombe  za  kienyeji  pamoja, sema  tu  leo  wamefumwa  wakijivinjari  ndo  mwanamke  anamsingizia  eti  kambaka,” alisema  shuhuda  mmoja.
 
Juhudi  za  kumpata  Kingwendu  kuongelea  mkasa  huo  hazikuzaaa  matunda  kutokana  na  simu  yake  kutopatikana  kila  akipigiwa

Kituko kingine alichofanya Balotelli uwanjani hiki hapa

 Baada ya kukaa kimya kwa muda mfupi, staa wa soka asiyeisha vituko Mario Balotelli amerudi tena kwenye ‘headlines’ za vyombo vya habari ulimwenguni.
Balotelli ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani akijiandaa na msimu mpya kwa pamoja na wachezaji wenzie wa klabu ya AC Milan, jana wakiwa kwenye mechi ya pre season dhidi ya Manchester City, Balotelli akafanya kituko kingine kilichowaacha watu midomo wazi.
Wakati mchezo ukiwa unaendelea mashabiki wawili wa AC Milan waliingia uwanjani na kwenda moja kwa moja kumvamia Mario Balotelli, huku walinzi wakiwa wanawakimbiza kwa nyuma, mashabiki hao wawili walitoa simu na kumuomba Balotelli kupiga nae picha.

Balotelli alionyesha kufurahishwa na hilo suala na kutoa ushirikiano kwa mashabiki hao kwa kupozi nao na kupiga ‘selfie’ – kitendo ambacho kiliibua shangwe za kutosha kutoka mashabiki wengine waliojazana kwenye uwanja wa Pittsburgh.
Mchezo huo uliisha kwa Manchester City kuifunga AC Milan 5-1.

Cristian Ronaldo afunguka kuhusu kujiunga katika kampuni ya Lil Wayne

Baaada ya Jay Z kufungua kampuni ya ya kusimamia wanamichezo na kuanza kupata mafanikio kupitia biashara hiyo, mwanamuziki mwingine nguli wa hip hop kutoka nchini Marekani, Lil Wayne ameripotiwa kufungua kampuni ya usimamizi wa wanamichezo na Cristiano Ronaldo, ametajwa kuwa mchezaji wa kwanza kusainiwa na kampuni hiyo ya Wayne.
Taarifa zilizotoka mwanzoni mwa wiki hii zilisema Lil Wayne kupitia kampuni yake atakuwa akishughulikia masuala yote ya kibiashara ya Ronaldo ndani ya Marekani, kwa mujibu wa TMZ.
Kampuni hiyo ya Weezy’ inatajwa kuwa ingefanya kazi na kampuni ya PolarisSports, kampuni dada na CAA na GestiFute, taasisi ambayo wakala wa Ronaldo – Jorge Mendes ndio anaiendesha.
Lakini jana kupitia mtandao wa Twitter, Ronaldo alikanusha taarifa hizo za kuingia kwenye ushirikiano wa kibiashara na kampuni ya Wayne, huku akisisitiza timu yake ni ile ile na hajabadilisha chochote.
Ronaldo yupo chini ya kampuni ya usimamizi wa wachezaji ya GestiFute, ambayo pia inamwakilisha Jose Mourinho, Pepe, James Rodriguez, Moutinho, Falcao, Nani na wachezaji wengine wengi wa Ureno na Amerika ya kusini.

Meneja ashangazwa na utajiri unao kuwa fasta kwa Ney wa Mitego

Miezi miwili iliyopita msanii Ney wa mitego alianika utajiri wa ajabu zikiwemo nyumba nne na gari moja ya kisasa nissan murano!! Akichezesha taya na mwandishi wetu aliyekuwa manager wa ney amesema tangu aachane na ney miezi 7 iliyopita alikuwa hana hata nyumba moja ameshangaa kumuona ana nyumba nne ghafla lakini manager amesema inawezekana jamaa anatafuta kiki ili watu wanaomuita kwenye show wafikirie kumpa mpunga mrefu na si laki laki wanazolipwa kwenye fiesta! Amefunguka kwamba Ney kuwa na hizo nyumba basi itakuwa ni miujiza.

Watanzania watatu walioshikwa Kenya kwenye harakati za kujiunga na Al Shabaab.



Wanajeshi wa kupambana na ugaidi nchini Kenya (ATPU) wanawashikilia raia watatu wa Tanzania waliokamatwa wakijaribu kuvuka mpaka wa Somalia na Kenya ili kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab.
Kamanda wa Polisi Lamu Mashariki amethibitisha kukamatwa kwa watatu ambao wote wana umri chini ya miaka 22 ambao kwa sasa wanashikiliwa na maafisa wa kupambana na Magaidi Kiunga mpaka wa Kenya na Somalia ambapo baada ya uchunguzi kukamilika watafikishwa Mahakamani.
Kukamatwa kwa watatu hawa kunafikisha idadi ya vijana sita wa Kitanzania waliokamatwa nchini Kenya ambao wanatuhumiwa kujiunga na mtandao wa kigaidi ambapo wengine watatu wanashikiliwa kwenye gereza la Kamiti waliokamatwa Kiamboni.
Miongoni mwao ni Bakari na Daudi ambapo walipohojiwa wamesema >>> ‘Tumeambiwa kwamba Somalia kuna Waislamu na wako katika hali ngumu, kuna majeshi mengi yanawanyanyasa Waislamu kwa hiyo kama Muislamu inabidi uende kutoa support kwa ndugu zako, kutokana na imani yangu kujengeka katika dini ndio nikajikuta naunga safari’
Haya yanajiri baada ya vijana kadhaa wa Kenya kukamatwa mpakani walipokua wakifanya mpango kuvuka mpaka na kuingia Somalia vilevile msajili wa kundi la Al Shabaab amekamatwa akiwapeleka vijana wawili wa Mombasa kwenda kujiunga na Al Shabaab mjini Garisa.
Wakati huohuo Polisi wanawasaka vijana waliotumwa na Al Shabaab kwenye mataifa ya Kenya na Tanzania kusubiri kupewa maagizo ya kundi hilo kutekeleza mashambulizi.

Sunday, 27 July 2014

Hussein Machozi yamkuta makubwa baada ya kukutwa akila Uroda na Mke wa Mwanasiasa maarufu, Mombasa nchini Kenya

Lundo la vyombo vya habari nchini Kenya limeandika habari kuwa hitmaker wa ‘Kwaajili Yako’, Hussein Machozi amekamatwa akizini na mke wa mwanasiasa maarufu mjini Mombasa, Kenya.
Habari za kukamatwa akiwa na mwanamke huyo zimeenea kwa kasi nchini humo. Gazeti la The Star limedai kuwa Hussein alikuwa na uhusiano wa siri na wa muda mrefu na mwanamke huyo na mume wake alikuwa ameshtuka tayari na hivyo kuwawekea mtego.

Limedai kuwa wawili hao walikuwa wanachepuka kiasi cha kupanga kununua nyumba ya pamoja. Vyanzo vilivyoongea na gazeti hilo vimedai kuwa mwanasiasa huyo huwa husafiri mara nyingi na hivyo kumpa upenyo mke wake kusaliti ndoa yake.

Blog moja ya Mombasa imeandika:

Msanii Hussein Machozi Apokea Kichapo Cha Mbwa Na Kupewa Masaa 24 Kuondoka Hapa Nchini Kenya.

Msanii huyu mashuhuri wa bongo flavor leo hii katika hoteli flani ya kitalii hapa jijini Mombasa alijipata matatani baada ya kupatikana akiwa na mke wa kiongozi flani mashuhuri wa hapa nchini. 
 
Yasemekana mheshimiwa huyu amekua akimkulia timing Machozi bila mafanikio lakini leo siku arobaini zilitimia kwake msanii huyu mkosa adabu. Msanii huyu alipatikana red handed na mke wa kiongozi huyo kwa kitanda na hapo ndipo masaibu yakamkumba na kuamrishwa aondoke hapa nchini kwa masaa aliopewa.
 

Hii ni habari nzima ya gazeti la The Star:

Tanzania bongo artiste Hussein Machozi was caught pants down with the wife of a prominent Mombasa businessmen and beaten thoroughly. Hussein who is nursing injuries was at the coast to shoot a music video when he hooked up with the said wife.
 
According to multiple sources who requested anonymity, the singer has been in an alleged long standing secret affair with the married woman and they were planning on buying a house together.

To keep the affair alive, the two love birds shuffled between Dar es Salaam and Mombasa.

Our source told Word Is, “The married woman’s husband is a very busy man. His time is occupied by his numerous business ventures and politics. He started suspecting the wife is stepping out on him when he found funny texts on his wife’s WhatsApp. He then laid a trap for the two of them.”

The Tanzanian heartthrob fell into the trap and was caught with his hands in the cookie jar. Security teams on the ground tried to contain the fiasco as the husband of the wife rained blows on the star.
 
His closest friend Stephen Yaa famously known as Notystee – a Mombasa based promoter – was with the Hussein when he arrived in in Mombasa on Wednesday. Notystee confirmed to Word Is that the incident did happen and that the bongo act called him up saying that he was in trouble.
“I was shocked when I received a call from Hussein saying that he was in trouble. He had earlier told me that he was going to meet a certain lady whom he was in love with, but I didn’t knew what was going to happen,” Notystee said.
Commenting on the altercation, Hussein told Word Is, “I will get back (to Mombasa) when am well. I’m in great pain. I never knew that the lady belonged to a powerful man at the coast.” The star famed for singles like Kafia Ghetto and Addicted is currently hiding at one of the houses belonging to a prominent Tanzanian tycoon who lives in Nyali.

SHILOLE atamba kugombea ubunge Igunga 2015

SHILOLEShilole si mgeni katika kuota vitu vikubwa. Kutoka kwenye ndoto yake ya kufanya kolabo na Jennifer Lopez, awamu hii ameenda mbali zaidi.
 
 Muimbaji huyo amechoka ‘Kuchuna Mabuzi’ na sasa anataka kuingia mjengoni. Mrembo huyo ambaye jina lake halisi ni Zuwena Mohamed, amepanga kugombea ubunge kwenye jimbo analotokea la Igunga mkoani Tabora katika uchaguzi wa mwaka 2015!
Akizungumza kwenye kipindi na Sizi Kitaa cha Clouds TV, Shilole amesema yupo serious na nia hiyo na kama Mungu akipenda atakuwa mbunge wa jimbo hilo.
  “Baada ya Dokta Dalali Kafumu anayefuata ni mimi,” amesema Shilole.
“Mimi nadhani napenda jimbo langu na napenda wakazi wangu wa Igunga wananiona toka nakua mpaka sasa hivi, kwahiyo wanafurahi. Sasa wananiambia ‘sisi hatutaki kumpa mtu mwingine kiti hiki sasa wananipa changamoto. 

“Vitu viwili vya kwanza ambavyo nitavifanya nikiingia kwenye lile bunge nikiwa kama msanii, kwanza nitatetea haki za wasanii, cha pili Igunga yangu wapo wakazi wa Igunga vijana wapate kazi, yaani akina mama, wale mama lishe na wengine lazima wawe na kazi zao. Kwahiyo nitawatafutia kazi, nitajenga chuo cha muziki,” alijinadi muimbaji huyo.
 
Msanii SHILOLE katika POZI
“Mimi jimbo langu nalijua na nimekua pale mpaka nimekuwa mkubwa lazima nilitimize sitaki wananchi wangu wapate tabu. Mimi nadhani wanaoenda kugombea majimbo yasiyo ya kwao wanaweza fanya chochote, lakini kama ni wa hapo lazima itakuuma. 

“Lakini unakuta mtu wa Dar es salaam anakwenda kugombea Mtwara huko nani anamjua? Mimi nitaenda kugombea kwangu lazima nitapata kura lazima watanipa! Kwahiyo kaeni tayari Shilole ni mbunge mtarajiwa Igunga,” alitamba.

Jumuiya ya Ulaya yaamishia vikwazo kwa wakuu wa ujasusi Urusi


Ikighadhibishwa kutokana na kudunguliwa kwa ndege ya abiria ya Malaysia Umoja wa Ulaya imewaingiza kwenye orodha yake ya vikwazo wakuu wa ujasusi wa Urusi wakati ikijiandaa kuchukuwa hatua kali zaidi dhidi ya nchi hiyo.
Alexander Bortnikov Mkuu wa Shirika la Usalama la Urusi (FSB).
Kwa mujibu wa waraka rasmi ya Umoja wa Ulaya Mkurugenzi wa shirika la usalama la FSB Alexander Bortnikov na Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Kigeni la Urusi Mikhail Fradkov ni miongoni mwa watu 15 na asasi 18 zilizokumbwa na hatua za kuzuiliwa mali zao na marufuku ya viza.
Taarifa hiyo imesema Bortnikov na Fradkov ambao wote wawili ni wajumbe wa Baraza la Usalama la Urusi wamejumuishwa kwenye orodha hiyo kwa kuhusika na "kuitishia mamlaka ya dola,haki ya kujitawala na uhuru wa Ukraine."
Waathirika kwa vikwazo
Miongoni mwa watu wengine waliojumuishwa kwenye vikwazo hivyo ni Rais Ramzan Kadyrov wa Chehchnya kwa kupendekeza kutuma vikosi vyake kuwasaidia waasi wanaoiunga mkono Urusi mashariki mwa Ukraine ambao wamelaumiwa kwa kuiangusha ndege hiyo ya Malaysia safari nambari MH 17 kwa kutumia kombora lililotengenezwa Urusi.
Rais wa Chechnya Ramzan Kadyrov amejumuishwa kwenye vikwazo vya Umoja wa Ulaya.
Makundi yaliyoingizwa kwenye vikwazo hivyo ni wanamgambo waasi, mamlaka zilioko Ukraine pamoja na kampuni zinazotajwa kusaidia na kurahisisha kunyakuliwa kwa rasi ya Crimea na Urusi hapo mwezi wa Machi ambako ndiko iliko kambi ya manowari za Urusi katika Bahari Nyeusi.
Maafisa wa Umoja wa Ulaya wamesema orodha ya majina zaidi inatarajiwa kutolewa hapo Jumanne yumkini ikawalenga watu waliko karibu na Rais Vladimir Putin wa Urusi.
Tangazo hilo lililotolewa Jumamosi (26.07.2014) inamaanisha jumla ya watu 87 na asasi 20 zimekumbwa na awamu ya pili ya vikwazo ya kuzuwiya mali na marufuku za viza vya Umoja wa Ulaya wakati ukijiandaa kupitisha awamu ya tatu ya vikwazo itakayokuwa pana zaidi kwa kulenga sekta kuu za uchumi.
Vikwazo vikali zaidi
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Umoja wa Ulaya katika mkutano wa Brussels.(22.07.2014)
Wawakilishi wa nchi wanachama 28 wa Umoja wa Ulaya walikubaliana hapo Ijumaa juu ya waraka wa kisheria wa kuwezesha utekelezaji wa hatua hizo mpya zenye kulenga nyanja nne masoko ya mtaji, ulinzi, matumizi ya bidhaa kwa pande mbili na teknolohjia nyeti ikiwemo sekta ya nishati.
Wawakilishi hao na maafisa wa serikali wataendelea kujadiliana mwishoni mwa juma na Jumatatu kwa lengo la kukamilisha mkutano wao wa mwisho hapo Jumanne.
Kwa kawaida viongozi wa Umoja wa Ulaya watakutana ili kutowa baraka zao za kisiasa lakini Rais wa Baraza la Ulaya Herman Van Rompuy tayari amewataka katika baruwa kuwaagiza mabalozi wao kukubali hatua hizo hapo Jumanne.
Mpango wa vikwazo unafaa
Jose Manuel Barroso Mkuu wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya.
Mkuu wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso amesema hapo Ijumaa mpango huo wa vikwazo iliopendekezwa unafaa,shabaha zake ni mahsusi una uwiano na unaweza kufanyiwa mabadiliko ya kutosha kuuwezesha Umoja wa Ulaya kuurekebisha kwa kulingana na hali ya mambo yanavyokwenda.
Barosso pia amerudia wito uliokuwa ukitolewa kwa Urusi kubadili mkondo wake kwa Ukraine ,kuwacha kuwasaidia waasi na kujitolea kwa mazungumzo makini ya kutafuta ufumbuzi wa amani kwa mzozo huo.
Hadi sasa kutokana na ukweli kwamba nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Ulaya zina uhusiano mkubwa wa kiuchumi na Urusi zimeufanya umoja huo kusita kuchukuwa hatua kali za kiuchumi zinazoungwa mkono na Marekani lakini kudunguliwa kwa ndege ya Malaysia kulikogharimu takriban maisha ya watu 300 kumeufanya ubadili msimamo huo.
Uchumi wa Urusi k
Katika baruwa yake Van Rompuy amesema hatua hizo zitakuwa na taathira kubwa kwa uchumi wa Urusi lakini athari haitokuwa kubwa kwa uchumi wa Ulaya ambao bado uko katika mchakato wa kufufuka.
Vikwazo vya silaha vilivyopendekezwa vitaathiri mikataba ya usoni tu na kuiepusha Ufaransa na tahayuri kutokana na mauzo yake ya meli mbili za kivita chapa ya Mistral yenye thamani ya euro bilioni 1.2 yaliokosolewa mno.
Katika sekta ya teknolojia vikwazo hivyo vitawekwa katika sekta ya mafuta na sio gesi ambapo kwayo Urusi husambaza theluthi moja ya mahitaji ya Ulaya na hii ni kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa nishati wa Umoja wa Ulaya.
Urusi imekuwa ikishutumu vikwazo hivyo vya Marekani na Umoja wa Ulaya kuwa havifai, havileti tija na vina madhara kwa maslahi yao ya pamoja hususan kutokana na vitisho vya ugaidi vinavyozidi kuongezeka na ukosefu wa utulivu duniani.
Imerudia tena ujumbe wake huo Jumamosi kwa kusema Umoja wa Ulaya umetamka kwa vitendo lakini kwa kuhatarisha ushirikiano wa kimataifa katika fani ya usalam

Uingereza yaibania Urusi kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2018

FIFA yaikabidhi Urusi haki za kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018.
Naibu waziri mkuu nchini Uingereza Nick Clegg ametoa wito wa Urusi kupokonywa haki za kuandaa mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2018.
Ameliambia gazeti la Sunday Times kwamba haiwezekani kwa michuano hiyo kufanyika nchini humo kufuatia hatua ya Urusi kuwaunga mkono waasi wa Ukraine mashariki mwa taifa hilo wanaoushukiwa kwa kuitungua ndege ya abiria ya Malaysia hivi majuzi.
Amesema kuwa ulimwengu utaonekana myonge iwapo utaruhusu michuano hiyo kuendelea nchini Urusi.
Urusi imelaumu Ukraine kwa kuanguka kwa ndege hiyo iliowauawa takriban watu 300.

Daktari wa ugonjwa wa Ebola naye afariki dunia kwa ugonjwa huo


Idara ya afya nchini Liberia imetangaza kuwa Daktari mmoja wa Ebola amefariki kutokana na viini vya ugonjwa huo.
Ni daktari wa kwanza nchini humo kufariki kutokana na ugonjwa huo tangu uzuke mapema mwaka huu.
Daktari Samuel Brisbane aliambukizwa viini vya ugonjwa huo alipokuwa akiwatibu wagonjwa wa Ebola katika mji mkuu wa Monrovia.
Alihudumu kama daktari wa watu wengi maarufu akiwemo rais wa zamani Charles Taylor.
Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa takriban watu 660 wamethibitishwa ama wanashukiwa kufariki na ugonjwa huo Magharibi mwa Afrika tangu mwezi February na kuufanya kuwa ugonjwa m'baya zaidi tangu uzuke.

Gaza kimenuka tena Israel yaamua kuendeleza mashambulizi kama kawa




Jeshi la Israel limesema kuwa linaendeleza mashambulizi yake katika eneo la Gaza .
Hatua hiyo inajiri baada ya wapiganaji wa Kipalestina Hamas kurusha takriban makombora 20 nchini Israel licha ya makubaliano ya kusitisha vita kuongezwa kwa masaa mengine 12 kufuatia ombi la Umoja wa Mataifa.
Kundi la Hamas limesema kuwa halitasita kutekeleza mashambulizi hadi wanajeshi wa Israel watakapoondoka ndani ya maeneo ya Palestina.
Mwanajeshi mmoja wa Israel anadaiwa kuuawa na shambulizi la roketi usiku kucha.
Siku ya jumamosi raia wengi wa Gaza walitumia fursa ya kusitishwa kwa vita hivyo kutembelea maeneo mengi yalioharibiwa karibu na mpaka na Israel huku miili ya raia wa Palestina waliouawa ikiendelea kufukuliwa kutoka kwa vifusi vya majengo yalioharibiwa.

Saturday, 26 July 2014

MOURINHO:Wamebugi hatuwezi kutumia pesa za klabu ovyo kama wao kwa kulipa asiye staili................




Chelsea ambao walitaka kumsajili  Luke Shaw dirisha dogo la  January lakini hawakufanikiwa baada ya kugundua angewaghalimu pesa nyingi.
Badala yake  Louis Van Gaal akamkalibisha Manchester United kwa pouni 27m akiwa ni kinda la miaka19 akiwa mchezaji wa timu ya Taifa la uingereza analipwa mshahara wa pouni 100,000 kwa wiki.
Mourinho badala yake akafanikiwa kumsajili mchezaji wa kimataifa mwenye asili ya Brazir Filipe Luis, 28,kwa kiasi kidogo cha mshaala ambao alikuwa akilipwa awali huku kocha uyo akikili kuwa kama angemsajili Shaw kwa kiasi ambacho kilikuwa mezani Pouni 50m basi angebadili hali ya hewa  katika chumba cha kubadilishia nguo cha Chelsea au klabu ingekumbwa na lungu la matumizi mabaya pesa.
“Kama tungemlipa chipukizi wa miaka 19 kama tulivyotakiwa kufanya kwa Luke Shaw tungekuwa kufa.
 “Tungejiua wenyewe katika matumizi mabaya na hali katika vyumba vya kubadilishia nguo ingekuwa mbaya sana”alisema Mourinho.
Alisema endapo utamlipa chipukiza pesa nyingi mwenye kiwango bora, ni sawa, lakini kwa kiwango hicho itakuwaje kwa siku zijazo? Kwa kuwa kunachipukizi ambao kila kukicha vipaji vyao vinaibuka.
‘’Kama utamlipa pesa nyingi kinda wa miaka 19 akiwa ni mchezaji mzuri ni sawa,lakini kama utaendelea kwa mtindo huo kwa wachezaji makinda itakuwaje baadae kwa kuwa  kunachipukizi wengi ambao vipaji vyao vinaibuka.”alisema Mourinho.
 .“Watasema kuwa,Itawezekana vipi?nimekuwa katika klabu hii zaidi  na kufanikiwa kucheza zaidi ya mechi 200 na kushinda makombe kibao,itawezekana vipi kinda la miaka 19 aje hapa apate pesa zaidi  yangu,?
Alisema kuwa kama  hali hiyo itaruhusiwa katika klabu hiyo inaweza kupelekea uchumi wa klabu kupolomoka.
‘’Unaweza kusema Filipe hana thamani ,huku wapenzi  wa  mpira Brazir wanampenda Filipe acheze katika kikosi cha timu hiyo hata hivyo ameshisha Ligi ya Spain La liga,ameshinda mashindano ya Ulaya,na kacheza klabu bingwa nusu fainali,lakini huyu anaonekana anathamani ndogo kuliko kinda la hapa uingereza,katika  wastani  wetu wa malipo ya mshahara  yeye ndio sahihi kwetu ’’alisema Mourinho.