Tuesday, 17 March 2015

Ndege ya BA yatua kutokana na harufu ya Choo



Hama  kweli duniani hakuishi vituko..! hivi karibuni  kumeripotiwa kutokea  kwa ndege moja ya shirika la ndege la British Airways kulazimika kutua kufuatia harufu mbaya iliyokuwa ikitokea  chooni.
Ndege hiyo  aina ya BA ilikuwa ikielekea Heathrow Uingereza kutoka Dubai safari ambayo kwa kawaida huchukua saa saba hadi kufika.
Abiria mmoja aliyekuwa ndani ya ndege hiyo aliyejulikana kama  Abhishek Sachdev, aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuwa
''Amini usiamini ndege yetu ya British Airways imelazimika kurejea dubai baada ya wahudumu kugundua kuwa harufu mbaya inatokea kwenye choo cha ndege hiyo.
“Yamkini rubani wa ndege hiyo aliwaita msimamizi wa wahudumu wa ndege hiyo ndipo tukang'amua kuwa kulikuwa na tashwishi katika safari yetu” Sachdev alinukuliwa na gazeti moja.
Anasema walielezwa na  rubani kuwa harufu mbaya ndani ya ndege hiyo inatokana na choo cha ndege hiyo kuwa kichafu na kwamba ilikuwa ni ya kinyesi.
Sachdev anasema hadi kufikia wakati huo ilikuwa takribani nusu saa tangu ndege hiyo ipae angani hivyo ikalamika kujerea nchini Dubai na ikawapasa kusubili zaidi ya saa 15 kwa kuwa hapakuwa na mbadala wa kurejea London.
Kwa upande wake mwakilishi wa ndege hiyo Greg James, Sarah, aliiambia Radio 1 kuwa jambo hilo halikuwa suala la kufanyiwa utani kwani ukiwa ndani ya ndege ni tishio kubwa kwa afya ya rubani na abiria kwa jumla.
''Ndani ya ndege huwa kunautupu wa hewa kwa hivyo asili mia 50 ya hewa inayotumika ni ileile kwa hivyo harufu mbaya ingeathiri vibaya afya ya abiria ndio sababu ndege hiyo haikuwa na budi ila kurejea iliisafishwe''.alisema.
Hata hivyo shirika hilo la ndege liliomba msamaha kwa usumbufu wowote kwa abiria wake walioathirika siku hiyo.

No comments:

Post a Comment