MAJAJI
watatu nchini Uingereza wamefutwa kazi
kwa kutumia muda wao ofisini kutizama filamu za ngono.
Wakitajwa
majina kuwa ni Jaji Timothy Bowles anayesikiza kesi za wilaya , jaji wa maswala
ya uhamiaji Warren Grant na jaji Peter Bullock kuwa wamefutwa kazi.
Kwa
mujibu wa wachunguzi wa idara ya mahakama
walithibitisha kuwa Majaji hao walipatikana na hatia ya kutumia mtandao rasmi wa mahakama hiyo.
Maafisa hao wanasemekana kuwa Majaji hao walitazama
mitandao yenye filamu za ngono huku wakifahamu vyema kuwa ilikuwa ni ukiukaji
wa sheria za matumizi kwa mujibu wa msimamizi wa idara hiyo ya Mahakama.
Hata
hivyo kiongozi wa idara ya mahakama hiyo ya Uingereza na jaji mkuu waliwapata
na hatia ya kwenda kinyume cha maadili ya mahakama.
Jaji wa nne
Andrew Maw aliamua kustaafu mwenyewe wakati uchunguzi huo ukiendelea badala ya
kufikishwa kizimbani.Mwandishi mmoja wa maswala ya kisheria anayejulikana kama Clive Coleman anasema kuwa makosa hayo yalikuwa makubwa sana katika mizani ya uadilifu wa majaji.
Aidha imefahamika kuwa hakuna hata mmoja wao atakayeruhusiwa kufanya kazi katika idara ya mahakama tena.
No comments:
Post a Comment