Tuesday, 17 March 2015

Kufeli hesabu kumetibua harusi nchini India





KATIKA muendelezo wa vituko duniani harusi moja ilitibuka nchini India baada ya bwana harusi kufeli swali rahisi sana la hisibati aliloulizwa na bi harusi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa kihoja hicho cha aibu kinachosemekana kutokea wakati  bi harusi alipomuuliza swali  bwana harusi kwamba ‘15 ukiongeza 6 utapata nini’ na bwana huyo hasijue cha kujibu.
Hata hivyo polisi katika jimbo hilo la Uttar Pradesh nchini India wanasema kuwa sherehe za harusi hiyo zilitibuka baada ya bi harusi kufoka mumewe mtarajiwa alipotoa jibu lake kuwa  ''17 ''.
Ni mara nyingi maharusi hukutana kwa mara ya kwanza katika sherehe za harusi yao.
Cha kushangaza ni pale bi harusi alikurupuka na kuondoka jukwaani akiwa amenuna  huku akisema hawezi kuoa mtu ambaye hakwenda shuleni.Hivyo juhudi zote za ndugu na jamaa pamoja na marafiki waliofika katika eneo hilo kushuhudia ziliambulia patupu.
Na baadae polisi katika jimbo hilo walisema kuwa jamaa wa bwana na bi harusi wote walikubaliana kurejesheana zawadi zote walizokuwa wametoa kwaajili ya wapendwa hao.
Ifahamike kuwa asilimia kubwa ya ndoa zote nchini India hupangwa na wazazi na mara nyingi maharusi hukutana kwa mara ya kwanza katika sherehe za harusi yao hivyo Baba yake  bi harusi Mohar Singh ambaye ndiye aliyekuwa amepanga harusi hiyo katika kijiji cha Rasoolabad akiongea na waandishi alidai kuwa  mwanawe alishangaa  mumewe mtarajiwa Ram Baran hakuwa msomi.
Katika tukio linalofanana na hilo nchini humo lilitokea mwezi uliopita bi harusi mwengine aliolewa na mgeni katika harusi yake baada ya Mumewe aliyekuwa amepanga kumuoa kuanguka kifafa dakika chache tu kabla ya wawili hao kuunganishwa kuwa mume na mke .

No comments:

Post a Comment