Friday, 12 December 2014

'Ujenzi wa maabara wakwamishwa na uhaba wa wataalamu'







MKUU wa Mkoa wa Da er Salaam Said Meck Sadik ametoa agizo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kuwatafuta na kuwaajili mafundi sadifu wa maabara ili kuharakisha ujenzi  huo.
Hali hiyo imetokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete la kila  shule ya sekondali ya Serikali iwe na maabara ya Biolojia,Kemia na Fzikia huku Mkoa wa Dar es Salaam ukiwa na Shule za Serikali 135 na kutakiwa kuwa na maabara 405.
Hayo aliyazungumza jana,jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari alisema hali hiyo imetokana na kuwapo kwa mafundi wa wataalam wa maabara  saba katika shule 135 za sekondari.
Alisema kutokana na tatizo hilo Manispaa zitawajibika kuwatafuta wataalam waliostaafu ili kuwaajili ikiwa lengo ni kupunguza uhaba huo pamoja na kuharakisha ujenzi.
“Kutokana na uhaba huu watalaam watafutwe popote na waajiliwe kutokana na ujuzi wao japokuwa jambo ili litakuwa gumu kwa upande wa mikoani lakini mijini halitasumbua kwa kuwa baadhi yao wanaendelea kujishughulisha na taaluma hiyo, ”alisema.
Aidha alisema kuwa miongoni mwa changamoto nyingine zilizojitokeza ambazo zinadaiwa kuzotesha ujenzi huo pamoja na ukosefu wa umeme, maji na mabeseni ya maabara.
Hata hivyo Mkuu huyo amesema kuwa ametoa maagizo kwa halmashauri  kutafuta  ufumbuuzi wa changamoto hizo.

No comments:

Post a Comment