Utaratibu huo utakaotumika katika siku ya
upigaji kura,kuesabu na kutangaza matokeo, umeelekezwa na kufanunuliwa na
kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka huu.
Hakitoa ufafanuzi juu ya utaratibu huo jana
jijini Dar es Salaam,Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Jumanne Sagin alisema wizara
imelazimika kutoa ufafanuzi huo ili kufahamisha Wananchi njia za kufuata katika
kupiga kura na kupunguza hali ya sintofahamu.
“Siku hiyo patakuwa na karatasi ya kura ambayo
itaandaliwa na halmashauri husika ikiwa na jina la mgombea,jina la chama,Nembo
ya halmashauri,na mpiga kura atatakiwa kutia alama ya vema katika kisanduku
kilichoko chini ya nembo ya chama ili kuonesha kuwa amempigia mgombea
aliyemtaka,”alisema Sagin.
Alisema utaratibu wa kupiga kura utaanza saa mbili
(2:00) asubuhi hadi saa kumi jioni ambapo wapiga kura watakao kuwapo kituoni
saa kumi (10:00) jioni wataruhusiwa kupiga kura hadi watakapokuwa wamemalizika.
Alisema Msimamizi Msaidizi atajirizisha kama
jina la limeorodheshwa katika orodha ya wapiga kura na baadae ataitaji mpiga
kura kuwa na kitambulisho chochote kabla
ya kupiga kura ili kumtambulisha yeye ni raia wa Tanzania.
“Ikiwa Mpiga kura hatakuwa na kitambulisho cha
aina yeyote lakini jina lake likaonekana katika orodha ya wapiga kura
iliyoandaliwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi,Msimamizi huyo atamruhusu kupiga
kura baada ya kutambuliwa na wakazi wa eneo hilo,”alisema Sagin
Akizungumzia katika Mikoa iliyofanya vizuri
katika uandikishwa wa wapiga kura Sagin
alisema Dar es Salaam ni miongoni mwa mikoa iliyofanya vibaya katika zoezi hilo
ikiwa na asilimia 43,halmashauri ya Wilaya ya Kilindi 21,Same 22.
Akizitaja Halmashauri zilizofanya vizuri ni
Katavi asilimia 79, Kagera 78, Kilimanjaro 50, katavi 107,Babati 101.
Pia Sagin alisema kuwa siku ya jumapili Disemba
14 wapiga kura waliojiandikisha katika
daftari la kupiga kura ni 11,491,661 ambao wanatarajiwa kupiga na kusisitiza
kuwa wananchi kujitokeza kupiga kura
bila hofu ya usalama.
No comments:
Post a Comment